Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 23:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Na watu wote wakaiendea nyumba ya Baali, wakaibomoa; wakavunjavunja madhabahu zake na sanamu zake, wakamwua Matani kuhani wa Baali mbele ya madhabahu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Halafu watu wote wakaenda kwenye nyumba ya Baali, wakaibomoa na kuzivunja madhabahu pamoja na sanamu zake. Kisha wakamuua Matani, kuhani wa Baali, mbele ya madhabahu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Halafu watu wote wakaenda kwenye nyumba ya Baali, wakaibomoa na kuzivunja madhabahu pamoja na sanamu zake. Kisha wakamuua Matani, kuhani wa Baali, mbele ya madhabahu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Halafu watu wote wakaenda kwenye nyumba ya Baali, wakaibomoa na kuzivunja madhabahu pamoja na sanamu zake. Kisha wakamuua Matani, kuhani wa Baali, mbele ya madhabahu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Watu wote wakaenda kwenye hekalu la Baali na kulibomoa. Wakavunjavunja madhabahu pamoja na sanamu, na kumuua Matani kuhani wa Baali mbele ya hayo madhabahu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Kisha watu wote wakaenda kwenye hekalu la Baali na kulibomoa. Wakavunjavunja madhabahu pamoja na sanamu na kumuua Matani kuhani wa Baali mbele ya hayo madhabahu.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 23:17
10 Marejeleo ya Msalaba  

Eliya akawaambia, Wakamateni hao manabii wa Baali, asiokoke hata mmoja. Wakawakamata; na Eliya akawachukua mpaka kijito cha Kishoni, akawaua huko.


Alipaondoa mahali pa juu, akazibomoa nguzo, akaikata hiyo Ashera; akaivunja vipande vipande ile nyoka ya shaba aliyoifanya Musa; maana hata siku zile wana wa Israeli walikuwa wakiifukizia uvumba; naye akaiita jina lake Nehushtani.


Wakazibomoa madhabahu za mabaali machoni pake; na sanamu za jua, zilizoinuliwa juu yake, akazikatakata; Maashera, sanamu za kuchonga, na za kusubu, akazivunjavunja, akaziponda kuwa mavumbi, akayamimina juu ya makaburi ya hao waliozichinjia dhabihu.


Akazibomoa madhabahu, akazipondaponda Maashera na sanamu kuwa mavumbi, akazikatakata sanamu zote za jua katika nchi yote ya Israeli, kisha akarejea Yerusalemu.


Nazo sanamu zitatoweka kabisa.


nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na maashera yao yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni; na jina lao lifutilieni mbali na mahali hapo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo