Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 22:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA kama nyumba ya Ahabu; kwa kuwa hao walikuwa washauri wake, baada ya kifo cha baba yake, hata aangamie.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu kama vile jamaa ya Ahabu ilivyofanya kwani hao ndio waliokuwa washauri wake baada ya kifo cha baba yake, hata aangamie.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu kama vile jamaa ya Ahabu ilivyofanya kwani hao ndio waliokuwa washauri wake baada ya kifo cha baba yake, hata aangamie.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu kama vile jamaa ya Ahabu ilivyofanya kwani hao ndio waliokuwa washauri wake baada ya kifo cha baba yake, hata aangamie.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Akafanya yaliyo maovu machoni pa Mwenyezi Mungu kama walivyokuwa wamefanya nyumba ya Ahabu, kwa kuwa baada ya kufa kwa baba yake, nyumba ya Ahabu ndio walikuwa washauri wake, kwa uangamivu wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Akafanya yaliyo maovu machoni pa bwana kama walivyokuwa wamefanya nyumba ya Ahabu, kwa kuwa baada ya kufa kwa baba yake nyumba ya Ahabu ndio waliokuwa washauri wake, kwa uangamivu wake.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 22:4
9 Marejeleo ya Msalaba  

Yeye naye akazifuata njia za nyumba ya Ahabu; kwa kuwa mamaye alikuwa mshauri wake katika kufanya maovu.


Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali.


Mawazo ya mwenye haki ni adili; Bali mashauri ya mtu mwovu ni hadaa.


Nenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.


Mwanangu, acha kusikia mafundisho, Ukitaka tu kuyaasi maneno ya maarifa.


Ndipo Nebukadneza akatuma watu kuwakusanya maamiri, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, majaji, mahakimu na wakuu wa wilaya zote, ili wahudhurie wakati wa kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha.


Ndipo Nebukadneza akastaajabu, akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia mawaziri wake, Je! Hatukutupa watu watatu, wakiwa wamefungwa, katikati ya moto? Wakajibu, wakamwambia mfalme, Kweli, Ee mfalme.


Kwa maana amri za Omri ndizo zishikwazo, na matendo yote ya nyumba ya Ahabu, nanyi mnakwenda katika mashauri yao; ili nikufanye kuwa ukiwa, na wenyeji waliomo humo kuwa zomeo; nanyi mtayachukua matukano waliyotukanwa watu wangu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo