Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Mambo ya Nyakati 22:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Ila Yehosheba, binti mfalme, akamtwaa Yoashi, mwana wa Ahazia, akamwiba miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa karibu kuuawa, akamweka yeye na yaya wake katika chumba cha kulala. Basi Yehosheba, binti mfalme Yehoramu, mkewe Yehoyada kuhani, (naye alikuwa dada yake Ahazia,) akamficha ili Athalia, asimwue.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Lakini Yehosheba, binti ya mfalme Yehoramu alimchukua Yoashi, akamtwaa kwa siri kutoka miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa karibu kuuawa. Alimficha yeye pamoja na yaya wake, katika chumba cha kulala. Hivyo Yehosheba, binti ya mfalme Yehoramu, mke wa kuhani Yehoadani, kwa sababu alikuwa dadaye Ahazia, alimficha Yoashi ili Athalia asimuue.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Lakini Yehosheba, binti ya mfalme Yehoramu alimchukua Yoashi, akamtwaa kwa siri kutoka miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa karibu kuuawa. Alimficha yeye pamoja na yaya wake, katika chumba cha kulala. Hivyo Yehosheba, binti ya mfalme Yehoramu, mke wa kuhani Yehoadani, kwa sababu alikuwa dadaye Ahazia, alimficha Yoashi ili Athalia asimuue.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Lakini Yehosheba, binti Mfalme Yehoramu, akamtwaa Yoashi mwana wa Ahazia kwa siri kutoka miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa karibu kuuawa. Akamweka Yoashi pamoja na yaya wake ndani ya chumba cha kulala. Kwa kuwa Yehosheba, aliyekuwa binti Mfalme Yehoramu, na pia alikuwa mke wa kuhani Yehoyada, alikuwa dada yake Ahazia, akamficha huyo mtoto ili Athalia asimuue.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Lakini Yehosheba, binti wa Mfalme Yehoramu, akamtwaa Yoashi mwana wa Ahazia kwa siri kutoka miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa karibu kuuawa. Akamweka Yoashi pamoja na yaya wake ndani ya chumba cha kulala. Kwa kuwa Yehosheba, aliyekuwa binti wa Mfalme Yehoramu, na pia alikuwa mke wa kuhani Yehoyada, alikuwa dada yake Ahazia, akamficha huyo mtoto ili Athalia asimuue.

Tazama sura Nakili

2 Mambo ya Nyakati 22:11
14 Marejeleo ya Msalaba  

Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu, nacho kiti cha enzi cha ufalme wake nitakiimarisha milele.

Lakini kwa ajili ya Daudi, BWANA, Mungu wake, akampa taa humo Yerusalemu, amwinue mwanawe baada yake, na kuufanya imara Yerusalemu;

Ila Yehosheba, binti wa mfalme Yehoramu, dada yake Ahazia, akamtwaa Yoashi mwana wa Ahazia, akamwiba miongoni mwa hao wana wa mfalme waliouawa, yeye na mlezi wake, na kuwatia katika chumba cha kulala; wakamficha usoni pa Athalia, basi kwa hiyo hakuuawa.

Walakini BWANA hakupenda kuiharibu nyumba ya Daudi, kwa sababu ya agano alilolifanya na Daudi, na kama alivyomwahidi kuwa atampa taa, yeye na wazao wake siku zote.

Basi Athalia, mama wa Ahazia, alipoona ya kuwa mwanawe amekufa, akainuka, akawaangamiza jamaa yote ya kifalme ya nyumba ya Yuda.

Akawako pamoja nao, amefichwa nyumbani mwa Mungu, miaka sita. Na Athalia akaitawala nchi.

Katika mwaka wa saba Yehoyada alijasiri, akawatwaa makamanda wa mamia, Azaria mwana wa Yerohamu, na Ishmaeli mwana wa Yehohanani, na Azaria mwana wa Obedi, na Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri, akapatana nao.

BWANA huyabatilisha mashauri ya mataifa, Huitangua mipango ya watu.

Maana hasira ya binadamu itakusifu, Masalio ya hasira utajifunga kama mshipi.

na huo mto utafurika vyura, nao watakwea juu na kuingia ndani ya nyumba yako, na ndani ya chumba chako cha kulala, na juu ya kitanda chako, na ndani ya nyumba ya watumishi wako, na juu ya watu wako, na ndani ya meko yako, na ndani ya vyombo vyako vya kukandia unga.

Hapana hekima, wala ufahamu, Wala shauri, juu ya BWANA.

BWANA asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, Usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake; ndivyo nitakavyotenda kwa ajili ya watumishi wangu, ili nisiwaharibu wote.

ili wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo