Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 20:30 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

30 Basi ukatulia ufalme wake Yehoshafati; kwa sababu Mungu wake alimstarehesha pande zote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Basi, Yehoshafati akatawala kwa amani, na Mungu akampa amani pande zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Basi, Yehoshafati akatawala kwa amani, na Mungu akampa amani pande zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Basi, Yehoshafati akatawala kwa amani, na Mungu akampa amani pande zote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Ufalme wa Yehoshafati ukawa na amani, kwa kuwa Mungu wake alikuwa amempa amani pande zote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Ufalme wa Yehoshafati ukawa na amani, kwa kuwa Mungu wake alikuwa amemstarehesha pande zote.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 20:30
12 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa, mfalme alipokuwa akikaa katika nyumba yake, hapo BWANA alipomstarehesha, asiudhiwe na adui zake waliomzunguka pande zote,


Na Yuda wote wakakifurahia kile kiapo; kwani wameapa kwa moyo wao wote, na kumtafuta kwa mapenzi yao pia; naye ameonekana kwao; naye BWANA akawastarehesha pande zote.


Tena utalala, wala hapana atakayekutia hofu; Naam, wengi watakutafuta uso wako.


Akitoa utulivu yeye, ni nani awezaye kuhukumia makosa? Akificha uso wake, ni nani awezaye kumtazama? Kama hufanyiwa taifa, au mtu mmoja, ni sawasawa;


Toka mbinguni ulitangaza hukumu; Nchi iliogopa, ikakaa kimya.


Njia za mtu zikimpendeza BWANA, Hata adui zake huwapatanisha naye.


Ulalapo hutaona hofu; Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu.


Nami nitawapa amani katika nchi, tena mtalala na hakuna atakayewatia hofu; nami nitawakomesha wanyama wabaya katika nchi yenu, wala hautapita upanga katika nchi yenu.


Mabaki ya Israeli hawatatenda uovu, wala kusema uongo; wala ulimi wa hadaa hautakuwa kinywani mwao; kwa maana watakula na kulala, wala hapana mtu atakayewatisha.


Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.


Hata ikawa baada ya siku nyingi, BWANA alipokuwa amekwisha kuwapa Israeli amani mbele ya adui zao pande zote, naye Yoshua alipokuwa mzee, mwenye miaka mingi sana,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo