Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 20:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

28 Wakafika Yerusalemu wenye vinanda, vinubi na parapanda kwenda nyumbani kwa BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Walipofika Yerusalemu, walikwenda moja kwa moja hadi nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakipiga vinanda, vinubi na tarumbeta.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Walipofika Yerusalemu, walikwenda moja kwa moja hadi nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakipiga vinanda, vinubi na tarumbeta.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Walipofika Yerusalemu, walikwenda moja kwa moja hadi nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakipiga vinanda, vinubi na tarumbeta.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Wakaingia Yerusalemu na kwenda hekaluni mwa Mwenyezi Mungu wakiwa na vinubi, zeze na tarumbeta.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Wakaingia Yerusalemu na kwenda hekaluni mwa bwana wakiwa na vinubi, zeze na tarumbeta.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 20:28
12 Marejeleo ya Msalaba  

Daudi na nyumba yote ya Israeli wakacheza mbele za BWANA kwa nguvu zao zote, kwa nyimbo, na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa kayamba, na kwa matoazi.


Wakacheza Daudi na Israeli wote, mbele za Mungu, kwa nguvu zao zote; na kwa nyimbo na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa matoazi, na kwa tarumbeta.


na elfu nne walikuwa mabawabu; na elfu nne walimsifu BWANA kwa vinanda, nilivyovifanya, alisema Daudi, vya kumsifia.


Hao wote waliamriwa na baba yao, waimbe nyumbani mwa BWANA, wakiwa na matoazi, vinanda, na vinubi, kwa utumishi wa nyumba ya Mungu; Asafu, Yeduthuni, na Hemani wakiwa wanaamriwa na mfalme.


Kisha wakarudi, kila mtu wa Yuda na Yerusalemu, na Yehoshafati mbele yao, ili kuurudia Yerusalemu kwa furaha; kwa kuwa BWANA amewafurahisha juu ya adui zao.


Ikawa hofu ya Mungu juu ya falme zote za nchi, waliposikia ya kuwa BWANA amepigana juu ya adui za Israeli.


Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa sauti tamu ya matari na kinubi.


Amka, ee moyo wangu. Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri.


Kwa chombo chenye nyuzi kumi, Na kwa kinanda, Na kwa mlio wa kinubi.


Njoni, tumwimbie BWANA, Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo