Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 20:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Wakaja watu waliomwambia Yehoshafati, wakisema, Wanakuja jamii kubwa juu yako watokao Shamu toka ng'ambo ya bahari; na tazama, wako katika Hasason-tamari (ndio Engedi).

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Watu kadhaa walikuja wakamwambia mfalme Yehoshafati, “Jeshi kubwa limekuja kukushambulia kutoka Edomu, ngambo ya Bahari ya Chumvi. Tayari wamekwisha teka Hasason-tamari.” (Hili ni jina lingine la Engedi).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Watu kadhaa walikuja wakamwambia mfalme Yehoshafati, “Jeshi kubwa limekuja kukushambulia kutoka Edomu, ngambo ya Bahari ya Chumvi. Tayari wamekwisha teka Hasason-tamari.” (Hili ni jina lingine la Engedi).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Watu kadhaa walikuja wakamwambia mfalme Yehoshafati, “Jeshi kubwa limekuja kukushambulia kutoka Edomu, ng'ambo ya Bahari ya Chumvi. Tayari wamekwisha teka Hasason-tamari.” (Hili ni jina lingine la Engedi).

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Watu fulani wakaja wakamwambia Yehoshafati, “Jeshi kubwa linakuja dhidi yako kutoka Shamu tokea ng’ambo ile nyingine ya Bahari. Tayari liko Hasason-Tamari” (yaani En-Gedi).

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Watu fulani wakaja wakamwambia Yehoshafati, “Jeshi kubwa linakuja dhidi yako kutoka Edomu tokea ng’ambo ile nyingine ya Bahari. Tayari liko Hasason-Tamari” (yaani En-Gedi).

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 20:2
10 Marejeleo ya Msalaba  

Hawa wote wakakutana katika bonde la Sidimu, yaani Bahari ya Chumvi.


Kisha wakarudi wakaja mpaka Enmisfati, ndio Kadeshi, wakapiga nchi yote ya Waamaleki, na Waamori waliokaa Hasason-tamari.


Mpendwa wangu ni kama kishada cha hina, Katika mizabibu huko Engedi.


Tena itakuwa, wavuvi watasimama karibu nao; toka Engedi mpaka En-eglaimu, patakuwa ni mahali pa kutandazia nyavu; samaki wao watakuwa namna zao mbalimbali, kama samaki wa bahari kubwa, wengi sana.


Na upande wa kusini, kuelekea kusini, utakuwa ni kutoka Tamari mpaka maji ya Meriba-Kadeshi, mpaka kijito cha Misri, mpaka bahari kubwa. Huu ndio upande wa kusini, kuelekea kusini.


Na mpakani mwa Gadi, upande wa kusini kuelekea kusini, mpaka wake utakuwa toka Tamari, mpaka maji ya Meriba-Kadeshi, mpaka kijito cha Misri, mpaka bahari kubwa.


kisha mpaka utateremkia Yordani, na kutokea kwake kutakuwa hapo katika Bahari ya Chumvi; hii ndiyo nchi yenu kama mipaka yake ilivyo kuizunguka pande zote.


na Nibshani, na huo Mji wa Chumvi, na Engedi; miji sita, pamoja na vijiji vyake.


ndipo hayo maji yaliyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa kichuguu, mbali sana, huko Adamu, mji ule ulio karibu na Sarethani, na maji yale yaliyoteremkia bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yataacha kutiririka kabisa; watu wakavuka kukabili Yeriko.


Naye Daudi akakwea kutoka huko, akakaa katika ngome ya Engedi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo