Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 2:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

3 Sulemani akatuma watu kwa Hiramu mfalme wa Tiro, akisema, Kama ulivyomtendea baba yangu Daudi, na kumletea mierezi, ajijengee nyumba ya kukaa, unitendee na mimi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Kisha, Solomoni akatuma ujumbe kwa Hiramu, mfalme wa Tiro, akamwambia, “Nitendee na mimi kama ulivyomtendea baba yangu Daudi, ulipompelekea mierezi ya kujengea ikulu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Kisha, Solomoni akatuma ujumbe kwa Hiramu, mfalme wa Tiro, akamwambia, “Nitendee na mimi kama ulivyomtendea baba yangu Daudi, ulipompelekea mierezi ya kujengea ikulu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Kisha, Solomoni akatuma ujumbe kwa Hiramu, mfalme wa Tiro, akamwambia, “Nitendee na mimi kama ulivyomtendea baba yangu Daudi, ulipompelekea mierezi ya kujengea ikulu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Sulemani akapeleka ujumbe huu kwa Mfalme Hiramu wa Tiro: “Unitumie magogo ya mwerezi kama ulivyomfanyia baba yangu Daudi wakati ulipompelekea mierezi ya kujenga jumba lake la kifalme la kuishi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Sulemani akapeleka ujumbe huu kwa Mfalme Hiramu wa Tiro: “Unitumie magogo ya mierezi kama ulivyomfanyia baba yangu Daudi wakati ulipompelekea mierezi ya kujenga jumba lake la kifalme la kuishi.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 2:3
18 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, akampelekea na mierezi, na maseremala, na waashi; nao wakamjengea Daudi nyumba.


Naye Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, akampelekea na mierezi, na waashi, na maseremala, ili wamjengee nyumba.


nao humtolea BWANA kila asubuhi, na kila jioni, sadaka za kuteketezwa na fukizo la manukato; mikate ya wonyesho pia huiweka kwa taratibu yake juu ya meza takatifu, na kinara cha dhahabu chenye taa zake, kuwaka kila jioni; kwa maana sisi tunayatunza maagizo ya BWANA, Mungu wetu; bali ninyi mmemwacha.


Nao walipomaliza, wakaleta mbele ya mfalme na Yehoyada fedha iliyobaki, na kwavyo vikafanywa vyombo vya nyumba ya BWANA, vyombo vya utumishi, navyo vya kutolea, na miiko, na vyombo vya dhahabu na fedha. Wakatoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya BWANA, mara kwa mara, siku zote za Yehoyada.


Basi Sulemani akavifanya vyombo vyote vilivyokuwamo nyumbani mwa Mungu, madhabahu ya dhahabu pia, nazo meza, ambazo juu yake iliwekwa mikate ya wonyesho;


kadiri ilivyohitajiwa huduma ya kila siku, akitoa sawasawa na amri ya Musa, siku za sabato, na za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoamriwa, mara tatu kila mwaka, yaani, sikukuu ya mikate isiyochachwa, na sikukuu ya majuma, na sikukuu ya vibanda.


Katika mwaka wa kwanza wa mfalme Koreshi, mfalme Koreshi alitoa amri, Kuhusu nyumba ya Mungu huko Yerusalemu, nyumba hiyo na ijengwe, mahali watoapo dhabihu, na misingi yake ipigwe na kufanywa imara sana; kuinuka kwake kuwe mikono sitini, na upana wake mikono sitini;


Kisha tukapiga kura, makuhani, na Walawi, na watu, juu ya matoleo ya kuni, ili kuzileta nyumbani kwa Mungu wetu, kwa kadiri ya mbari za baba zetu, kwa nyakati zilizoamriwa, mwaka kwa mwaka, kukoka moto madhabahuni mwa BWANA, Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika torati;


Nawe utaiweka mikate ya wonyesho juu ya meza mbele yangu daima.


Basi sadaka utakazozitoa juu ya madhabahu ni hizi; wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja kila siku.


Mwana-kondoo mmoja utamchinja asubuhi; na mwana-kondoo wa pili utamchinja jioni;


Na huyo mwana-kondoo wa pili utamchinja wakati wa jioni, na utamtoa dhabihu pamoja na sadaka ya nafaka na sadaka yake ya kinywaji kama asubuhi, ili itoe harufu nzuri, iwe dhabihu ya kusogeswa kwa Bwana kwa njia ya moto.


Na Haruni atafukiza uvumba wa manukato juu yake; kila siku asubuhi atakapozitengeneza zile taa, ataufukiza.


Nena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Sikukuu za BWANA, ambazo mtazitangaza kuwa ni makusanyiko matakatifu; hizi ni sikukuu zangu.


Kisha akaisongeza sadaka ya unga, na kutwaa konzi humo, na kuiteketeza juu ya madhabahu, pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi.


Tena katika mianzo ya miezi yenu mtamsogezea BWANA sadaka ya kuteketezwa; nayo ni ng'ombe dume wadogo wawili, na kondoo dume mmoja, na wana-kondoo wa kiume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, saba;


Tena katika siku ya Sabato watasongezwa wana-kondoo dume wawili, wa mwaka mmoja, wakamilifu, pamoja na sehemu ya mbili ya kumi za efa za unga laini kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, pamoja na sadaka yake ya kinywaji;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo