Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 15:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 Wakamwapia BWANA kwa sauti kuu, na kwa kelele, na kwa parapanda, na kwa baragumu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Walimwapia Mwenyezi-Mungu kwa sauti kuu, wakapaza sauti zaidi, wakapiga tarumbeta na baragumu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Walimwapia Mwenyezi-Mungu kwa sauti kuu, wakapaza sauti zaidi, wakapiga tarumbeta na baragumu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Walimwapia Mwenyezi-Mungu kwa sauti kuu, wakapaza sauti zaidi, wakapiga tarumbeta na baragumu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Wakamwapia Mwenyezi Mungu kwa sauti kuu, kwa kelele, na kupiga tarumbeta na mabaragumu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Wakamwapia bwana kwa sauti kuu, kwa kupiga kelele, tarumbeta na kwa mabaragumu.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 15:14
9 Marejeleo ya Msalaba  

na ya kwamba yeyote asiyemtafuta BWANA, Mungu wa Israeli, atauawa, akiwa mdogo au mkubwa, awe ni mwanamume au mwanamke.


Na Yuda wote wakakifurahia kile kiapo; kwani wameapa kwa moyo wao wote, na kumtafuta kwa mapenzi yao pia; naye ameonekana kwao; naye BWANA akawastarehesha pande zote.


wakaambatana na ndugu zao, wakuu wao, nao wakaingia katika laana na kiapo, ya kuwa wataiendea Torati ya Mungu, iliyotolewa kwa mkono wa Musa, mtumishi wa Mungu, na kuziangalia, na kuzitenda, amri zote za BWANA, Bwana wetu, na maagizo yake na sheria zake;


Tena nikakung'uta nguo yangu, nikasema, Mungu na amkung'ute vivyo hivyo kila mtu nyumbani mwake, na kazini mwake, asiyeitimiza ahadi hiyo; naam, na akung'utwe vivyo hivyo, na kuwa hana kitu. Mkutano wote wakasema, Amina; wakamhimidi BWANA. Nao watu wakafanya kama walivyoahidi.


Kwa panda na sauti ya baragumu. Shangilieni mbele za Mfalme, BWANA.


Musa akaenda akawaambia watu maneno yote ya BWANA, na hukumu zake zote; watu wote wakajibu kwa sauti moja, wakasema, Maneno yote aliyoyanena BWANA tutayatenda.


Kisha akakitwaa Kitabu cha Agano akakisoma masikioni mwa watu; wakasema, Hayo yote aliyoyanena BWANA tutayatenda, nasi tutatii.


Ndipo hao watu wakamwambia Yoshua, BWANA, Mungu wetu, ndiye tutakayemtumikia; na sauti yake ndiyo tutakayoitii.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo