Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 14:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Asa na watu waliokuwa pamoja naye wakawafuata mpaka Gerari; wakawaua Wakushi wengi sana asipone hata mmoja; kwa sababu waliangamizwa mbele za BWANA, na mbele ya jeshi lake; na hao wakachukua mateka wengi sana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Asa pamoja na wanajeshi wake wakawafuatilia mpaka Gerari, wakawaua Waethiopia wengi sana, asibaki hata mmoja, kwani walikuwa wamekwisha shindwa na Mwenyezi-Mungu pamoja na jeshi lake. Jeshi la Yuda lilichukua nyara nyingi sana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Asa pamoja na wanajeshi wake wakawafuatilia mpaka Gerari, wakawaua Waethiopia wengi sana, asibaki hata mmoja, kwani walikuwa wamekwisha shindwa na Mwenyezi-Mungu pamoja na jeshi lake. Jeshi la Yuda lilichukua nyara nyingi sana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Asa pamoja na wanajeshi wake wakawafuatilia mpaka Gerari, wakawaua Waethiopia wengi sana, asibaki hata mmoja, kwani walikuwa wamekwisha shindwa na Mwenyezi-Mungu pamoja na jeshi lake. Jeshi la Yuda lilichukua nyara nyingi sana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 naye Asa na jeshi lake wakawafuatia hadi Gerari. Idadi kubwa ya Wakushi ilianguka hata wasiweze kuinuka tena, wakapondapondwa mbele za Mwenyezi Mungu na majeshi yake. Watu wa Yuda wakachukua nyara nyingi sana;

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 naye Asa na jeshi lake wakawafuatia mpaka Gerari. Idadi kubwa ya Wakushi ilianguka hata wasiweze kuinuka tena, wakapondapondwa mbele za bwana na majeshi yake.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 14:13
17 Marejeleo ya Msalaba  

Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika.


Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha.


Abrahamu akaondoka huko kwenda nchi ya kusini, akakaa kati ya Kadeshi na Shuri, naye akatembea katika Gerari.


Ikawa njaa katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya kwanza iliyokuwa siku za Abrahamu. Isaka akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, huko Gerari.


Wakashika njia, hofu ya Mungu ikaishika miji iliyowazunguka, wala hawakuwafuata wana wa Yakobo.


Maana siku baada ya siku watu waliomwendea Daudi ili kumsaidia, hadi wakapata kuwa jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.


akiwa na magari elfu moja na mia mbili, na wapanda farasi elfu sitini; na watu wasiohesabika, waliotoka Misri pamoja naye; Walubi, na Wasukii, na Wakushi.


Wakaipiga miji yote kandokando ya Gerari; maana hofu ya BWANA ikawajia; nao wakaiteka nyara miji yote, kwa maana zilikuwamo ndani yake nyara nyingi mno.


Wakamchinjia BWANA siku ile, katika nyara walizozileta, dhabihu za ng'ombe mia saba, na kondoo elfu saba.


Hofu ya BWANA ikaziangukia falme za nchi zote zilizozunguka Yuda, wasipigane vita na Yehoshafati.


Ikawa hofu ya Mungu juu ya falme zote za nchi, waliposikia ya kuwa BWANA amepigana juu ya adui za Israeli.


Kwamba Mungu angekuwa radhi kuniponda; Kwamba angeulegeza mkono wake na kunikatilia mbali!


Yeye ni mwenye hekima moyoni, na mwenye uwezo katika nguvu; Ni nani aliyejifanya kuwa mgumu juu yake, naye akafanikiwa?


Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa? Wala, Ee Mungu, huendi na majeshi yetu?


watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake;


Akasema, La, lakini mimi ni kamanda wa jeshi la BWANA, nimekuja sasa. Yoshua akainama chini hadi nchi, akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake?


Nakuomba ulisamehe kosa lake mjakazi wako, kwa kuwa hakika BWANA atamfanyia bwana wangu nyumba iliyo imara, kwa sababu bwana wangu anavipiga vita vya BWANA; tena uovu hautaonekana ndani yako siku zako zote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo