Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 12:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

3 akiwa na magari elfu moja na mia mbili, na wapanda farasi elfu sitini; na watu wasiohesabika, waliotoka Misri pamoja naye; Walubi, na Wasukii, na Wakushi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 akiwa na magari 1,200, wapandafarasi 60,000, na askari wengi mno wasiohesabika, waliotoka Misri pamoja naye: Walibia, Wasukii na Waethiopia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 akiwa na magari 1,200, wapandafarasi 60,000, na askari wengi mno wasiohesabika, waliotoka Misri pamoja naye: Walibia, Wasukii na Waethiopia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 akiwa na magari 1,200, wapandafarasi 60,000, na askari wengi mno wasiohesabika, waliotoka Misri pamoja naye: Walibia, Wasukii na Waethiopia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Akiwa na magari ya vita elfu moja mia mbili, wapanda farasi elfu sitini, na idadi isiyohesabika ya majeshi ya Walibia, Wasukii na Wakushi waliokuja pamoja naye kutoka Misri.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Akiwa na magari ya vita 1,200 na wapanda farasi 60,000 na idadi isiyohesabika ya majeshi ya Walibia, Wasukii na Wakushi yaliyokuja pamoja naye kutoka Misri.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 12:3
15 Marejeleo ya Msalaba  

Wakakimbia Washami mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami, watu wa magari mia saba, na wapanda farasi elfu arubaini, naye akampiga huyo Shobaki, jemadari wa jeshi lao, hata akafa huko.


Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi.


Basi, BWANA akawapiga Wakushi mbele ya Asa, na mbele ya Yuda; na Wakushi wakakimbia.


Naye Asa alikuwa na jeshi waliochukua ngao na mikuki, katika Yuda elfu mia tatu; na katika Benyamini wenye kuchukua vigao na kupinda upinde, elfu mia mbili na themanini; hao wote walikuwa mashujaa.


Kisha, Zera Mkushi alikuja kuwashambulia akiwa na jeshi la watu milioni moja na magari mia tatu akaja Maresha.


Je! Hao Wakushi na Walubi hawakuwa jeshi kubwa mno, wenye magari na wapanda farasi wengi sana? Lakini, kwa kuwa ulimtegemea BWANA, aliwatia mkononi mwako.


Maana mimi ni BWANA, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, Mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako.


Kushi, na Putu, na Ludi, na watu wote waliochanganyika, na Kubu, na wana wa nchi ya agano, wataanguka kwa upanga pamoja nao.


Lakini atakuwa na nguvu juu ya hazina za dhahabu na fedha, na juu ya vitu vyote vya Misri vyenye thamani; na Walibya na Wakushi watafuata nyayo zake.


Kushi na Misri walikuwa nguvu zake, nazo zilikuwa hazina mpaka; Puti na Walibya walikuwa wasaidizi wake.


Na hesabu ya majeshi ya wapanda farasi ilikuwa milioni mia mbili; nilisikia hesabu yao.


Sisera akayakusanya magari yake yote, naam, magari ya chuma mia tisa, na watu wote waliokuwa pamoja naye, toka Haroshethi wa Mataifa mpaka mto wa Kishoni.


Kwa maana walikwea na ng'ombe zao na hema zao, wakaja mfano wa nzige kwa wingi; wao na ngamia zao pia walikuwa hawana hesabu; nao waliingia katika hiyo nchi ili kuiharibu.


Nao Wafilisti wakakusanyika ili wapigane na Waisraeli, magari elfu thelathini, na wapanda farasi elfu sita, na watu kama mchanga ulio ufuoni mwa bahari kwa wingi wao; wakapanda juu, wakapiga kambi yao katika Mikmashi, upande wa mashariki wa Beth-aveni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo