Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 12:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 Basi mambo yake Rehoboamu, ya kwanza hadi za mwisho, je! Hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu Shemaya nabii na Ido mwonaji, kwa jinsi ya kuandika nasaba? Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu siku zote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Matendo yote ya mfalme Rehoboamu ya mwanzo mpaka ya mwisho na rekodi ya ukoo yameandikwa katika kitabu cha Kumbukumbu za nabii Shemaya, na Kumbukumbu za Ido Mwonaji. Wakati huu wote, kulikuwa na vita vya mfululizo kati ya Rehoboamu na Yeroboamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Matendo yote ya mfalme Rehoboamu ya mwanzo mpaka ya mwisho na rekodi ya ukoo yameandikwa katika kitabu cha Kumbukumbu za nabii Shemaya, na Kumbukumbu za Ido Mwonaji. Wakati huu wote, kulikuwa na vita vya mfululizo kati ya Rehoboamu na Yeroboamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Matendo yote ya mfalme Rehoboamu ya mwanzo mpaka ya mwisho na rekodi ya ukoo yameandikwa katika kitabu cha Kumbukumbu za nabii Shemaya, na Kumbukumbu za Ido Mwonaji. Wakati huu wote, kulikuwa na vita vya mfululizo kati ya Rehoboamu na Yeroboamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Kwa habari ya matukio katika utawala wa Rehoboamu, kuanzia mwanzo hadi mwisho, je, hayakuandikwa katika kumbukumbu za nabii Shemaya na mwonaji Ido zinazohusiana na vizazi? Kulikuwa na vita vya mara kwa mara kati ya Rehoboamu na Yeroboamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Kwa habari ya matukio katika utawala wa Rehoboamu, tangu mwanzo mpaka mwisho, je, hayakuandikwa katika kumbukumbu za nabii Shemaya na mwonaji Ido zinazohusiana na vizazi? Kulikuwako na vita mara kwa mara kati ya Rehoboamu na Yeroboamu.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 12:15
13 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini likaja neno la Mungu kwa Shemaya mtu wa Mungu, kusema,


Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo hadi mwisho, angalia, zimeandikwa katika kumbukumbu za Samweli, mwonaji, na katika kumbukumbu za Nathani, nabii, na katika kumbukumbu za Gadi, mwonaji;


Lakini neno la BWANA likamjia Shemaya mtu wa Mungu, kusema,


Ndipo akaja Shemaya nabii kwa Rehoboamu, na kwa wakuu wa Yuda, waliokusanyika Yerusalemu kwa sababu ya Shishaki, akawaambia, BWANA asema hivi, Ninyi mmeniacha mimi, kwa hiyo nami nimewaacha ninyi mkononi mwa Shishaki.


Katika mwaka wa kumi na nane wa mfalme Yeroboamu, Abiya akaanza kutawala juu ya Yuda.


Miaka mitatu akatawala huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Maaka binti Urieli wa Gibea. Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.


Na mambo ya Abiya yaliyosalia, na njia zake, na maneno yake, yameandikwa katika kitabu cha maelezo cha nabii Ido.


Na tazama, mambo yake Asa, toka mwanzo hadi mwisho, angalia, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.


Na mambo yote ya Yehoshafati yaliyosalia, ya kwanza hadi mwisho, angalia, yameandikwa katika salua ya Yehu mwana wa Hanani, iliyotiwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli.


Basi mambo yake yote yaliyosalia, na njia zake zote, za kwanza hadi za mwisho, tazama, yameandikwa katika Kitabu cha Wafalme wa Yuda na Israeli.


na mambo yake, ya kwanza hadi ya mwisho, tazama, yameandikwa katika Kitabu cha Wafalme wa Israeli na Yuda.


Basi mambo yake Sulemani yaliyosalia, tangu mwanzo hadi mwisho je! Hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu la Nathani nabii, katika unabii wa Ahiya, Mshiloni, na katika maono ya Ido mwonaji ambayo yahusu Yeroboamu mwana wa Nebati?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo