Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 12:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Naye alipojinyenyekeza, ghadhabu ya BWANA ikamgeukia mbali, asimharibu kabisa; tena yalionekana katika Yuda mambo mema.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Alipojinyenyekesha, Mwenyezi-Mungu aliacha kumghadhibikia na hakumwangamiza kabisa. Zaidi ya hayo, hali ya nchi ya Yuda ilikuwa nzuri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Alipojinyenyekesha, Mwenyezi-Mungu aliacha kumghadhibikia na hakumwangamiza kabisa. Zaidi ya hayo, hali ya nchi ya Yuda ilikuwa nzuri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Alipojinyenyekesha, Mwenyezi-Mungu aliacha kumghadhibikia na hakumwangamiza kabisa. Zaidi ya hayo, hali ya nchi ya Yuda ilikuwa nzuri.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Kwa sababu Rehoboamu alijinyenyekeza, hasira ya Mwenyezi Mungu ikageukia mbali naye, hakuangamizwa kabisa. Kukawa na hali nzuri katika Yuda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Kwa sababu Rehoboamu alijinyenyekeza, hasira ya bwana ikageukia mbali naye, hakuangamizwa kabisa. Kukawa na hali nzuri katika Yuda.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 12:12
12 Marejeleo ya Msalaba  

Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hutauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo?


Na Israeli wote watamlilia, na kumzika, kwa maana ndiye peke yake wa Yeroboamu atakayeingia kaburini; kwa sababu limeonekana ndani yake jambo lililo jema kwa BWANA, Mungu wa Israeli, nyumbani mwa Yeroboamu.


Ikawa kila wakati mfalme alipoingia nyumbani mwa BWANA, wakaja walinzi wakazichukua, wakazirudisha tena chumbani mwa walinzi.


Walakini, yameonekana kiasi cha mema ndani yako, kwa kuwa umeyaondoa Maashera katika nchi, na moyo wako umeukaza kumtafuta Mungu.


Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.


Na ijapokuwa imebaki sehemu moja katika sehemu kumi ndani yake, italiwa hii nayo; kama mvinje na kama mwaloni, ambao shina lake limebaki, ingawa imekatwa; kadhalika mbegu takatifu ndiyo shina lake.


Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi.


Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.


Sisi tumekosa na kuasi; Wewe hukusamehe.


Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo