Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 1:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Sulemani akamwambia Mungu, Umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Solomoni akamwambia Mungu, “Ulimwonesha baba yangu Daudi fadhili nyingi, na umenijalia kuwa mfalme mahali pake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Solomoni akamwambia Mungu, “Ulimwonesha baba yangu Daudi fadhili nyingi, na umenijalia kuwa mfalme mahali pake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Solomoni akamwambia Mungu, “Ulimwonesha baba yangu Daudi fadhili nyingi, na umenijalia kuwa mfalme mahali pake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Sulemani akamjibu Mungu, “Umemwonesha baba yangu Daudi fadhili nyingi, nawe umeniweka niwe mfalme mahali pake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Sulemani akamjibu Mungu, “Umemwonyesha baba yangu Daudi fadhili nyingi, nawe umeniweka niwe mfalme mahali pake.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 1:8
13 Marejeleo ya Msalaba  

Yeye ni mnara wa wokovu kwa mfalme wake; Amfanyia fadhili masihi wake, Kwa Daudi na wazawa wake, hata milele.


Sulemani akasema, Umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu fadhili kuu, kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki, na katika unyofu wa moyo pamoja nawe; nawe umemwekea na fadhili hii kubwa, maana umempa mwana wa kuketi kitini pake kama ilivyo leo.


Ndipo akaingia Daudi mfalme, akaketi mbele za BWANA; akasema Mimi ni nani, Ee BWANA Mungu, na nyumba yangu ni nini, hata umenileta hadi hapa?


tena katika wana wangu wote (kwani BWANA amenipa wana wengi), amemchagua Sulemani mwanangu ili aketi juu ya kiti cha enzi cha ufalme wa BWANA, juu ya Israeli.


Ndipo Sulemani akaketi katika kiti cha enzi cha BWANA, awe mfalme badala ya Daudi babaye, akafanikiwa; nao Israeli wote wakamtii.


Akafa akiwa mzee sana, mwenye maisha marefu, mali na heshima; naye Sulemani mwanawe akatawala badala yake.


Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana; Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.


Bwana, ziko wapi fadhili zako za kwanza, Ulizomwapia Daudi kwa uaminifu wako?


Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo