Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wathesalonike 2:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

7 bali tulikuwa wapole katikati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 ingawa sisi tukiwa mitume wa Kristo, tungeweza kudai mambo fulani kwenu. Lakini sisi tulikuwa wapole kati yenu kama alivyo mama kwa watoto wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 ingawa sisi tukiwa mitume wa Kristo, tungeweza kudai mambo fulani kwenu. Lakini sisi tulikuwa wapole kati yenu kama alivyo mama kwa watoto wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 ingawa sisi tukiwa mitume wa Kristo, tungeweza kudai mambo fulani kwenu. Lakini sisi tulikuwa wapole kati yenu kama alivyo mama kwa watoto wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Lakini tulikuwa wapole kati yenu, kama vile mama anawatunza watoto wake wadogo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 lakini tulikuwa wapole katikati yenu, kama mama anayewatunza watoto wake wadogo.

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 2:7
18 Marejeleo ya Msalaba  

Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani mwake, Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.


Na wafalme watakuwa baba zako walezi, na malkia zao mama zako walezi; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni BWANA, tena waningojeao hawatatahayarika.


Mfano wa mtu ambaye mama yake amfariji, ndivyo nitakavyowafariji ninyi; nanyi mtafarijiwa katika Yerusalemu.


Je! Ni mimi niliyewatungisha mimba watu hawa wote je! Ni mimi niliyewazaa, hata ikawa wewe kuniambia, Haya, wachukue kifuani mwako, mfano wa baba mwenye kulea achukuavyo mtoto anyonyaye, uende nao mpaka nchi uliyowaapia baba zao?


Na kwa muda wa miaka kama arubaini akawavumilia katika jangwa.


Nami nilikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na kwa kutetemeka sana.


Kwa wanyonge nilikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu.


Basi, mimi Paulo mwenyewe nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo; mimi niliye mnyenyekevu nikiwapo pamoja nanyi, bali nisipokuwapo ni mwenye ujasiri kwenu;


Maana, alisulubiwa katika udhaifu, lakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Maana sisi nasi tu dhaifu katika yeye; lakini tutaishi pamoja naye kwa uweza wa Mungu ulio kwenu.


Watoto wangu wadogo, ambao nawaonea uchungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu;


vile vile, kama mjuavyo, jinsi tulivyomwonya kila mmoja wenu kama baba awaonyavyo watoto wake mwenyewe, tukiwatia moyo na kushuhudia;


Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo