Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wathesalonike 1:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaziacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai, wa kweli;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Watu hao wanazungumza juu ya ziara yetu kwenu: Jinsi mlivyotukaribisha, jinsi mlivyoziacha sanamu, mkamgeukia Mungu aliye hai na wa kweli,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Watu hao wanazungumza juu ya ziara yetu kwenu: Jinsi mlivyotukaribisha, jinsi mlivyoziacha sanamu, mkamgeukia Mungu aliye hai na wa kweli,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Watu hao wanazungumza juu ya ziara yetu kwenu: jinsi mlivyotukaribisha, jinsi mlivyoziacha sanamu, mkamgeukia Mungu aliye hai na wa kweli,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Kwa maana watu wa maeneo hayo wenyewe wanaeleza jinsi mlivyotupokea na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai na wa kweli,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Kwa maana watu wa maeneo hayo wenyewe wanaeleza jinsi mlivyotupokea na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaacha sanamu, ili kumtumikia Mwenyezi Mungu aliye hai na wa kweli,

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 1:9
30 Marejeleo ya Msalaba  

Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu?


Nafsi yangu imezionea shauku nyua za BWANA, Naam, na kuzikondea. Moyo wangu na mwili wangu Vinamlilia Mungu aliye hai.


Tega sikio lako, BWANA, usikie; funua macho yako, BWANA, uone; uyasikie maneno ya Senakeribu, aliyopeleka ili kumtukana Mungu aliye hai.


Yamkini BWANA, Mungu wako, atayasikia maneno ya huyo kamanda ambaye mfalme wa Ashuru, bwana wake, amemtuma ili amtukane Mungu aliye hai; na BWANA, Mungu wako atayakemea maneno aliyoyasikia; basi, inua dua yako kwa ajili ya mabaki yaliyobakia.


Bali BWANA ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele; Mbele za ghadhabu yake nchi yatetemeka, Wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake.


Ee BWANA, nguvu zangu, ngome yangu, na kimbilio langu siku ya taabu, kwako wewe watakuja mataifa yote toka ncha za dunia, wakisema, Baba zenu hawakurithi kitu ila uongo, naam, ubatili na vitu visivyofaa.


Mimi ninaweka amri, ya kwamba katika mamlaka yote ya ufalme wangu watu watetemeke na kuogopa mbele za Mungu wa Danieli; maana yeye ndiye Mungu aliye hai, adumuye milele, na ufalme wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata mwisho.


Tena itakuwa ya kwamba hesabu ya wana wa Israeli itafanana na mchanga wa bahari, usioweza kupimwa wala kuhesabiwa; tena itakuwa, badala ya kuambiwa, Ninyi si watu wangu, wataambiwa, Ninyi ndio wana wa Mungu aliye hai.


BWANA atakuwa wa kutisha sana kwao; kwa maana atawaua kwa njaa miungu yote ya dunia; na watu watamsujudia yeye, kila mtu toka mahali pake; naam, nchi zote za mataifa.


Kwa maana tokea maawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika mataifa; na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika mataifa, asema BWANA wa majeshi.


Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.


wakisema, Akina bwana, mbona mnafanya haya? Sisi nasi tu wanadamu hali moja na ninyi; tunawahubiria Habari Njema, ili mgeuke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo;


Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa, Ninyi si watu wangu, Hapo wataitwa wana wa Mungu aliye hai.


Mwajua ya kuwa mlipokuwa watu wa Mataifa, mlichukuliwa kufuata sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa.


Maana katika watu wote ni nani aliyeisikia sauti ya Mungu aliye hai, akisema toka kati ya moto, kama vile sisi, asife?


Maana ninyi wenyewe, ndugu, mnakujua kuingia kwetu kwenu, ya kwamba hakukuwa bure;


Kwa sababu hiyo sisi nasi tunamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe wa Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na kwa kweli ndivyo lilivyo; litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini.


kwa maana twajitaabisha na kujitahidi kwa kusudi hili, kwa sababu tunamtumaini Mungu aliye hai, aliye Mwokozi wa watu wote, hasa wa wale waaminio.


Bali ninyi mmeufikia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,


Yoshua akasema, Kwa jambo hili mtajua ya kuwa Mungu aliye hai yu kati yenu, na ya kuwa hatakosa kuwatoa mbele yenu Mkanaani, na Mhiti, na Mhivi, na Mperizi, na Mgirgashi, na Mwamori, na Myebusi.


Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu kutoka kwa sanamu.


ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wameleweshwa kwa mvinyo ya uasherati wake.


Daudi akaongea na watu waliosimama karibu, akisema, Je! Atafanyiwaje yeye atakayemwua Mfilisti huyo, na kuwaondolea Israeli aibu hii? Maana Mfilisti huyu asiyetahiriwa ni nani hata awatukane majeshi ya Mungu aliye hai?


Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo