Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 7:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Lakini kama Bwana alivyomgawia kila mtu, kama Mungu alivyomwita kila mtu, na aende vivyo hivyo. Ndivyo ninavyoagiza katika makanisa yote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Kwa vyovyote kila mmoja na aishi kufuatana na vipaji alivyogawiwa na Bwana, na kama alivyoitwa na Mungu. Hili ndilo agizo langu kwa makanisa yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Kwa vyovyote kila mmoja na aishi kufuatana na vipaji alivyogawiwa na Bwana, na kama alivyoitwa na Mungu. Hili ndilo agizo langu kwa makanisa yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Kwa vyovyote kila mmoja na aishi kufuatana na vipaji alivyogawiwa na Bwana, na kama alivyoitwa na Mungu. Hili ndilo agizo langu kwa makanisa yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Lakini kila mtu na aishi maisha aliyopangiwa na Bwana Isa, yale Mungu aliyomwitia. Hii ni sheria ninayoiweka kwa makundi yote ya waumini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Lakini kila mtu na aishi maisha aliyopangiwa na Bwana Isa, yale Mwenyezi Mungu aliyomwitia. Hii ni sheria ninayoiweka kwa makundi yote ya waumini.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 7:17
18 Marejeleo ya Msalaba  

Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.


Msiwakoseshe Wayahudi wala Wagiriki wala kanisa la Mungu,


Lakini mtu yeyote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu.


mtu akiwa na njaa, na ale nyumbani kwake; msipate kukutanika kwa hukumu. Na hayo yaliyosalia nikija nitayatengeneza.


Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.


Kuhusu ile michango kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo hivyo.


Kwa sababu hii nimemtuma Timotheo kwenu, aliye mwanangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakayewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama vile nifundishavyo kila mahali katika kila kanisa.


Je! Mtu fulani ameitwa akiwa amekwisha kutahiriwa? Asijifanye kana kwamba hakutahiriwa. Mtu fulani ameitwa akiwa hajatahiriwa bado? Basi asitahiriwe.


Ndugu zangu, kila mtu na akae mbele za Mungu katika hali iyo hiyo aliyoitwa nayo.


Ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; lakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi.


Mbali na mambo ya nje, yako yanijiayo kila siku, ndiyo maangalizi ya makanisa yote.


Na pamoja naye tukamtuma ndugu yule ambaye sifa zake katika Injili zimeenea makanisani kote.


Lakini sikujulikana uso wangu na makanisa ya Yudea yaliyokuwa katika Kristo;


Maana ninyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Yudea, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu wenyewe, waliyoyapata na hao kwa Wayahudi;


Hata na sisi wenyewe tunaona fahari juu yenu katika makanisa ya Mungu kwa ajili ya subira yenu, na imani mliyo nayo katika adha zenu zote na dhiki mnazostahimili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo