Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 15:55 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

55 Kuko wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? Uko wapi, Ewe mauti, uchungu wako?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

55 “Kifo, ushindi wako uko wapi? Uwezo wako wa kuumiza uko wapi?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

55 “Kifo, ushindi wako uko wapi? Uwezo wako wa kuumiza uko wapi?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

55 “Kifo, ushindi wako uko wapi? Uwezo wako wa kuumiza uko wapi?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

55 “Kuko wapi, ee mauti, kushinda kwako? Uko wapi, ee mauti, uchungu wako?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

55 “Kuko wapi, ee mauti, kushinda kwako? Uko wapi, ee mauti, uchungu wako?”

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 15:55
16 Marejeleo ya Msalaba  

Katika shingo yake hukaa nguvu, Na utisho hucheza mbele yake.


Ni mwanamume gani atakayeishi asione mauti, Atakayejiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu?


Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili.


Hakuna mwenye uwezo juu ya roho aizuie roho; Wala hana mamlaka juu ya siku ya kufa; Wala hakuna kuponyoka katika vita vile; Wala uovu hautamwokoa yule aliyeuzoea.


Nitawakomboa kwa nguvu za kaburi; nitawaokoa kutoka kwa mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Huruma itafichika machoni mwangu.


Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Abrahamu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.


Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu; Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu.


Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayemtesa.


lakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja.


Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati.


Nao wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi mitano ilikuwa katika mikia yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo