Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wakorintho 12:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Kama vile mwili ulivyo mmoja wenye viungo vingi, na viungo hivyo vyote – ingawaje ni vingi – hufanya mwili mmoja, ndivyo ilivyo pia kwa Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Kama vile mwili ulivyo mmoja wenye viungo vingi, na viungo hivyo vyote – ingawaje ni vingi – hufanya mwili mmoja, ndivyo ilivyo pia kwa Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Kama vile mwili ulivyo mmoja wenye viungo vingi, na viungo hivyo vyote — ingawaje ni vingi — hufanya mwili mmoja, ndivyo ilivyo pia kwa Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Kama vile mwili ulivyo mmoja nao una viungo vingi; navyo viungo vyote vya mwili ingawa ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Al-Masihi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Kama vile mwili ulivyo mmoja nao una viungo vingi, navyo viungo vyote vya mwili ingawa ni vingi, ni mwili mmoja, vivyo hivyo na Al-Masihi.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 12:12
16 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.


Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja.


Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na kila mmoja wenu akiwa kiungo cha mwili huo.


Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.


Basi ahadi zilinenwa kwa Abrahamu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazawa, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo.


ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.


kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;


Kuna mwili mmoja, na Roho mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.


Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.


Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake.


Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.


Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake;


wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukineemeshwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kama atakavyo Mungu.


Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo