Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wafalme 8:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 Mfalme akageuza uso wake, akawabariki mkutano wote wa Israeli; na mkutano wote wa Israeli wakasimama.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Kisha, Solomoni akaigeukia jumuiya yote ya Waisraeli wakiwa wamesimama, akawabariki,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Kisha, Solomoni akaigeukia jumuiya yote ya Waisraeli wakiwa wamesimama, akawabariki,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Kisha, Solomoni akaigeukia jumuiya yote ya Waisraeli wakiwa wamesimama, akawabariki,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Kusanyiko lote la Israeli walipokuwa wamesimama hapo, mfalme akageuka na kuwabariki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kusanyiko lote la Israeli lilipokuwa limesimama hapo, mfalme akageuka na kuwabariki.

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 8:14
14 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha Daudi alipokwisha kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani akawabariki watu kwa jina la BWANA wa majeshi.


Na Daudi alipokwisha kuitoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la BWANA.


Hata walipokuja Hezekia na wakuu, na kuyaona yale mafungu, wakamhimidi BWANA, na watu wake Israeli.


Mfalme akageukia mkutano wote wa Israeli akawabariki, mkutano wote wa Israeli ukiwa umesimama.


Makuhani wakasimama kwenye nafasi zao walipoagizwa; Walawi nao pamoja na vinanda vya BWANA, alivyovifanya Daudi mfalme, ili kumshukuru BWANA, kwa maana fadhili zake ni za milele, hapo aliposifu Daudi kwa mikono yao; nao makuhani wakapiga panda mbele yao; nao Israeli wote wakasimama.


Tena Yeshua, na Bani, na Sherebia, na Yamini, na Akubu, na Shabethai, na Hodai, na Maaseya, na Kelita, na Azaria, na Yozabadi, na Hanani, na Pelaya, nao ni Walawi, wakawafahamisha watu torati; na watu wakasimama mahali pao.


Waliokuwa wa wazao wa Israeli wakajitenga na wageni wote, wakasimama, wakaziungama dhambi zao, na maovu ya baba zao.


Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la BWANA; Tumewabariki toka nyumbani mwa BWANA.


Watu wote wakaiona nguzo ya wingu ikisimama penye mlango wa hema; watu wote wakaondoka wakasujudu, kila mtu mlangoni pa hema yake.


Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda katika mashua, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani.


Basi Yoshua akawabariki, na kuwapa ruhusa waende zao; nao wakaenda mahemani kwao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo