1 Wafalme 7:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC
14 Naye alikuwa mwana wa mwanamke mjane wa kabila la Naftali, na babaye alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba; naye alikuwa mwingi wa hekima na akili, stadi wa kufanya kazi zote za shaba. Akamfikia mfalme Sulemani, akamfanyia kazi yake yote.
14 Huyo, alikuwa mwana wa mjane wa kabila la Naftali, na baba yake alikuwa mkazi wa Tiro, mfua shaba. Hiramu alikuwa na hekima nyingi na akili, na fundi stadi wa kazi yoyote ya shaba. Basi, alikuja kwa mfalme Solomoni, akamfanyia kazi yake yote.

14 ambaye mama yake alikuwa mjane kutoka kabila la Naftali na baba yake alikuwa mtu wa Tiro tena fundi wa shaba. Hiramu alikuwa na ustadi wa hali ya juu na mzoefu katika aina zote za kazi ya shaba. Alikuja kwa Mfalme Sulemani na kufanya kazi zake zote alizopangiwa.

mwana wa mwanamke wa kabila la Dani, na babaye alikuwa mkazi wa Tiro, yeye ni bingwa wa kutumia dhahabu, fedha, shaba, chuma, mawe na mti; na wa nguo za urujuani, samawati, nyekundu na kitani safi; tena ni stadi kwa kutia nakshi na kuchora michoro yoyote, mbunifu na kuchora chochote kufuatana na kielekezo ambacho angepewa yeye na watu wako mastadi wa bwana wangu Daudi baba yako.
Lakini ni nani awezaye kumjengea nyumba, ikiwa mbingu hazimtoshi, wala mbingu za mbingu? Nami ni nani basi, hata nimjengee nyumba, isipokuwa kwa ajili ya pahali pa kufukizia mafusho mbele zake?
Vyungu, pia sepetu, nyuma na vyombo vingine vyote, Huram-abi akamtengenezea mfalme Sulemani kwa ajili ya nyumba ya BWANA, vilikuwa vya shaba iliyong'arishwa.
Amewajaza watu hao ujuzi, ili watumike katika kazi za kila aina, mawe, na kazi ya fundi mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri, ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yoyote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.
Basi Bezaleli na Oholiabu watatenda kazi, na kila mtu mwenye moyo wa hekima, ambaye BWANA amemtia akili na hekima ili ajue kufanya kazi hiyo yote kwa huo utumishi wa mahali patakatifu, kama hayo yote BWANA aliyoyaagiza.
Basi kila mtu mwenye moyo wa hekima miongoni mwa hao waliofanya kazi, akaifanya hiyo maskani ya mapazia kumi; ya nguo ya kitani nzuri ya kusokotwa, na nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu; pamoja na makerubi, kazi ya fundi stadi; ndivyo alivyoyafanya.