Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wafalme 6:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 Akayaweka hayo makerubi katika nyumba ya ndani; na mabawa ya makerubi yakanyoshwa, bawa la moja likafika ukutani huko, na bawa la kerubi la pili likafika ukutani huko; mabawa yao yakagusana katikati ya nyumba.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Sanamu hizo zilikuwa sambamba, zikiwa na mabawa yaliyokunjuliwa: Bawa la mmoja likigusa ukuta mmoja, na bawa la mwingine likigusa ukuta wa pili, huku yale mengine yaligusana katikati ya chumba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Sanamu hizo zilikuwa sambamba, zikiwa na mabawa yaliyokunjuliwa: Bawa la mmoja likigusa ukuta mmoja, na bawa la mwingine likigusa ukuta wa pili, huku yale mengine yaligusana katikati ya chumba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Sanamu hizo zilikuwa sambamba, zikiwa na mabawa yaliyokunjuliwa: bawa la mmoja likigusa ukuta mmoja, na bawa la mwingine likigusa ukuta wa pili, huku yale mengine yaligusana katikati ya chumba.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Aliwaweka makerubi hao katika chumba cha ndani kabisa cha Hekalu, mabawa yao yakiwa yamekunjuliwa. Bawa la kerubi mmoja liligusa ukuta mmoja, wakati bawa la yule mwingine liligusa ukuta wa upande mwingine, nayo mabawa yao mengine yaligusana katikati ya chumba.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Aliwaweka makerubi hao ndani ya Patakatifu pa Patakatifu pa Hekalu, mabawa yake yakiwa yamekunjuliwa. Bawa la kerubi mmoja liligusa ukuta mmoja, wakati bawa la yule mwingine liligusa ukuta mwingine, nayo mabawa yao mengine yaligusana katikati ya chumba.

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 6:27
8 Marejeleo ya Msalaba  

Kwenda juu kwake kerubi moja kulikuwa mikono kumi, na kerubi la pili vivyo hivyo.


Akayafunika makerubi kwa dhahabu.


Makuhani wakalileta sanduku la Agano la BWANA hadi mahali pake, katika chumba cha ndani cha ile nyumba, patakatifu pa patakatifu, naam, chini ya mbawa za makerubi.


Kwa maana makerubi yalinyosha mbawa zao, juu ya mahali pa sanduku, makerubi yakalifunika lile sanduku na miti yake kwa juu.


Na mabawa ya makerubi hayo urefu wake ulikuwa mikono ishirini; bawa moja mikono mitano, likiufikia ukuta wa nyumba; na bawa la pili mikono mitano, likishikana na bawa la kerubi la pili.


Kwa maana makerubi yalinyosha mabawa yao juu ya mahali pa sanduku, makerubi yakalifunika lile sanduku na miti yake kwa juu.


Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema.


Na hayo makerubi yakayanyosha mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zilikuwa zaelekeana hili kwa hili; nyuso za hayo makerubi zilikuwa zikielekea kiti cha rehema.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo