Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wafalme 22:39 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

39 Na mambo yote ya Ahabu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, na nyumba ya pembe aliyoijenga, na miji yote aliyoijenga, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

39 Matendo mengine ya mfalme Ahabu, jinsi alivyojenga na kupamba nyumba yake kwa pembe, na miji yote aliyojenga, yote yameandikwa katika Kitabu cha Mambo ya Nyakati ya Wafalme wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

39 Matendo mengine ya mfalme Ahabu, jinsi alivyojenga na kupamba nyumba yake kwa pembe, na miji yote aliyojenga, yote yameandikwa katika Kitabu cha Mambo ya Nyakati ya Wafalme wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

39 Matendo mengine ya mfalme Ahabu, jinsi alivyojenga na kupamba nyumba yake kwa pembe, na miji yote aliyojenga, yote yameandikwa katika Kitabu cha Mambo ya Nyakati ya Wafalme wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

39 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Ahabu, pamoja na yote aliyoyafanya, jumba la kifalme alilojenga na kupambwa kwa pembe za ndovu, nayo miji aliyoijengea ngome, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

39 Kwa matukio mengine ya utawala wa Ahabu, pamoja na yote aliyoyafanya, jumba la kifalme alilojenga na kupambwa kwa pembe za ndovu, nayo miji aliyoijengea maboma, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 22:39
16 Marejeleo ya Msalaba  

Tena mfalme akafanya kiti cha enzi kikubwa cha pembe, akakifunikiza kwa dhahabu iliyo safi.


Kwa kuwa mfalme alikuwa na merikebu za Tarshishi baharini pamoja na merikebu za Hiramu; mara moja katika miaka mitatu huja merikebu za Tarshishi, zikileta dhahabu, na fedha, na pembe, na nyani, na tausi.


Na mambo yake Yeroboamu yaliyosalia, ya kupigana na ya kutawala, tazama, yameandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli.


Na mambo yote ya Asa yaliyosalia, na nguvu zake zote, na yote aliyoyafanya, na miji aliyoijenga, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Yuda? Lakini alipokuwa mzee alikuwa na ugonjwa wa miguu.


Basi mambo yote ya Nadabu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli?


Na mambo yote ya Zimri yaliyosalia na fitina yake aliyoifanya, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli?


Nayo mambo yote ya Omri yaliyosalia aliyoyatenda, na uthabiti alioufanya, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli?


Basi, mambo yote ya Baasha yaliyosalia, na aliyoyafanya, na nguvu zake, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli?


Basi Ahabu akalala na baba zake; na Ahazia mwanawe akatawala mahali pake.


Na mambo yote yaliyosalia aliyoyafanya Ahazia, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli?


Basi mambo yote ya Shalumu yaliyosalia, na njama alizozifanya, tazama, yameandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli.


Mavazi yako yote hunukia manemane Na udi na mdalasini. Katika majumba ya pembe Vinubi vimekufurahisha.


Wadedani walikuwa wachuuzi wako, visiwa vingi vilikuwa soko la mkono wako; walikuletea pembe, na mpingo, ili kuvibadili.


kwa mialoni ya Bashani wamefanya makasia yako; na sitaha zako wamezifanya kwa pembe iliyotiwa kazi ya njumu katika mti wa mihugu itokayo Kitimu.


Nami nitaipiga nyumba ya wakati wa baridi pamoja na nyumba ya wakati wa joto; na hizo nyumba za pembe zitaangamia, nazo nyumba kubwa zitakuwa na mwisho, asema BWANA.


ninyi mnaolala juu ya vitanda vya pembe, na kujinyosha juu ya makochi yenu; ninyi mnaokula wana-kondoo wa kundi, na ndama waliomo zizini;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo