Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wafalme 21:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

16 Ikawa Ahabu aliposikia ya kwamba Nabothi amekufa, akaondoka, aliteremkie shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli, ili alitamalaki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Mara tu Ahabu aliposikia Nabothi amekwisha fariki, aliinuka kwenda kulimiliki shamba la mizabibu la Nabothi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Mara tu Ahabu aliposikia Nabothi amekwisha fariki, aliinuka kwenda kulimiliki shamba la mizabibu la Nabothi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Mara tu Ahabu aliposikia Nabothi amekwisha fariki, aliinuka kwenda kulimiliki shamba la mizabibu la Nabothi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Ahabu aliposikia Nabothi amekufa, akainuka, kisha akashuka kwenda kulimiliki shamba la mizabibu la Nabothi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Ahabu aliposikia Nabothi amekufa, akainuka na kushuka ili kulichukua shamba la mizabibu la Nabothi.

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 21:16
14 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa baada ya hayo, Nabothi Myezreeli alikuwa na shamba la mizabibu katika Yezreeli, karibu na nyumba ya kifalme ya Ahabu mfalme wa Samaria.


Ikawa Yezebeli aliposikia ya kwamba Nabothi amepigwa kwa mawe na kufa, Yezebeli akamwambia Ahabu, Inuka, ulitamalaki shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli, alilokataa kukupa kwa fedha, maana Nabothi hayuko hai, lakini amekufa.


Neno la BWANA likamjia Eliya Mtishbi, kusema,


Naye alipofika kilimani, alivichukua kutoka mikononi mwao, akaviweka nyumbani; akawaacha wale watu kuondoka, nao wakaenda zao.


Yoramu akasema, Tandika gari. Wakalitandika gari lake. Yoramu mfalme wa Israeli akatoka, na Ahazia mfalme wa Yuda, kila mtu katika gari lake. Wakatoka ili kumlaki Yehu, wakamkuta katika kiwanja cha Nabothi, Myezreeli.


Ulipomwona mwizi ulikuwa radhi naye, Ukashirikiana na wazinzi.


Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akung'utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za umwagaji wa damu; afumbaye macho yake asitazame uovu.


ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.


wakiiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa ujira wa udhalimu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo