Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wafalme 2:33 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

33 Hivyo damu yao itarudi kichwani pa Yoabu, na kichwani pa wazao wake hata milele; ila kwa Daudi, na kwa wazao wake, na kwa nyumba yake, na kwa kiti chake cha enzi, kutakuwa na amani hata milele kutoka kwa BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

33 Adhabu ya mauaji hayo itakuwa juu ya Yoabu na wazawa wake milele. Bali Mwenyezi-Mungu atawapa ufanisi daima, Daudi na wazawa wake watakaokalia kiti chake cha enzi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

33 Adhabu ya mauaji hayo itakuwa juu ya Yoabu na wazawa wake milele. Bali Mwenyezi-Mungu atawapa ufanisi daima, Daudi na wazawa wake watakaokalia kiti chake cha enzi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

33 Adhabu ya mauaji hayo itakuwa juu ya Yoabu na wazawa wake milele. Bali Mwenyezi-Mungu atawapa ufanisi daima, Daudi na wazawa wake watakaokalia kiti chake cha enzi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

33 Hatia ya damu yao na iwe juu ya kichwa cha Yoabu na wazao wake milele. Lakini kwa Daudi na uzao wake, nyumba yake na kiti chake cha ufalme, iwepo amani ya Mwenyezi Mungu milele.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

33 Hatia ya damu yao na iwe juu ya kichwa cha Yoabu na wazao wake milele. Lakini kwa Daudi na uzao wake, nyumba yake na kiti chake cha ufalme, iwepo amani ya bwana milele.”

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 2:33
24 Marejeleo ya Msalaba  

Reubeni akajibu, akawaambia, Sikuwaambia, nikisema, Msimkosee kijana? Wala hamkusikia; kwa hiyo tunadaiwa damu yake.


Ndipo huyo mwanamke wa Tekoa akamwambia mfalme, Na uwe juu yangu, Ee bwana wangu mfalme, na juu ya nyumba ya baba yangu uovu huu; wala kwa mfalme na kwa kiti chake cha enzi pasiwepo hatia.


Naye BWANA atamrudishia damu yake kichwani pake mwenyewe, kwa kuwa aliwapiga watu wawili wenye haki, na wema kuliko yeye, akawaua kwa upanga, wala babangu Daudi hakujua habari hiyo; yaani Abneri, mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Israeli, na Amasa, mwana wa Yetheri, jemadari wa jeshi la Yuda.


Tena, mfalme akamwambia Shimei, Umejua uovu wote uliouona moyoni mwako, uliomtenda Daudi baba yangu; basi kwa hiyo BWANA atakurudishia uovu wako kichwani pako mwenyewe.


basi, usikie huko mbinguni, ukatende, ukawahukumu watumwa wako; ukimpatiliza mtu mbaya, kwa kuleta njia yake juu ya kichwa chake; na kumpa mwenye haki haki yake, ukimjalia kwa kadiri ya haki yake.


Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji.


nawe sasa umekuwa radhi kuibarikia nyumba ya mtumishi wako, ipate kudumu milele mbele zako; kwa maana wewe, BWANA, umebarikia, nayo imebarikiwa milele.


Kila asubuhi nitawaangamiza Waovu wote nchini. Nikiwatenga wote watendao uovu Na mji wa BWANA.


Wanao wakiyashika maagano yangu, Na shuhuda nitakazowafundisha; Watoto wao nao wataketi Katika kiti chako cha enzi milele.


Alikuomba uhai, ukampa, Muda mrefu wa siku nyingi, milele na milele.


Wazao wake nao nitawadumisha milele, Na kiti chake cha enzi kama siku za mbingu.


Mwondoe asiye haki mbele ya mfalme, Na kiti chake cha enzi kitathibitika katika haki.


Basi Bwana MUNGU asema hivi; Kama mimi niishivyo, hakika kiapo changu alichokidharau, na agano langu alilolivunja, nitampatiliza kichwani pake.


Lakini kama hamtaki kufanya neno hilo, ninyi mmefanya dhambi mbele za BWANA, nanyi jueni ya kwamba hiyo dhambi yenu itawapata, hapana budi.


Watu wote wakajibu wakasema, Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu.


Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.


Walipopingana naye na kumtukana Mungu, akakung'uta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu; mimi ni safi; tangu sasa nitakwenda kwa watu wa Mataifa.


ili kwamba huo udhalimu waliotendewa hao wana sabini wa Yerubaali ulipizwe, ili damu yao iwe juu ya Abimeleki ndugu yao, aliyewaua, na juu ya watu wa Shekemu, waliomtia nguvu mikono yake ili awaue hao nduguze.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo