Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wafalme 2:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

29 Akaambiwa mfalme Sulemani ya kwamba, Yoabu amekimbilia Hemani kwa BWANA, naye, tazama, yuko madhabahuni. Ndipo Sulemani akamtuma Benaya, mwana wa Yehoyada, akisema, Nenda, umuue.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Mfalme Solomoni aliposikia kwamba Yoabu yumo katika hema la Mungu na kwamba amesimama madhabahuni, alimtuma Benaya mwana wa Yehoyada, akisema, “Nenda ukampige.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Mfalme Solomoni aliposikia kwamba Yoabu yumo katika hema la Mungu na kwamba amesimama madhabahuni, alimtuma Benaya mwana wa Yehoyada, akisema, “Nenda ukampige.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Mfalme Solomoni aliposikia kwamba Yoabu yumo katika hema la Mungu na kwamba amesimama madhabahuni, alimtuma Benaya mwana wa Yehoyada, akisema, “Nenda ukampige.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Mfalme Sulemani akaambiwa kuwa Yoabu amekimbilia kwenye hema la Mwenyezi Mungu naye alikuwa kando ya madhabahu. Basi Sulemani akamwagiza Benaya mwana wa Yehoyada: “Nenda ukamuue!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Mfalme Sulemani akaambiwa kuwa Yoabu amekimbilia kwenye hema la bwana naye alikuwa kando ya madhabahu. Basi Sulemani akamwagiza Benaya mwana wa Yehoyada: “Nenda ukamuue!”

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 2:29
9 Marejeleo ya Msalaba  

na Benaya, mwana wa Yehoyada, alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi; nao wana wa Daudi wakawa makuhani.


Mfalme Sulemani akatuma kuwa jambo hilo liwe mkononi mwa Benaya mwana wa Yehoyada: naye akampiga, hata akafa.


Basi Benaya akaja Hemani kwa BWANA, akamwambia, Mfalme asema hivi, Njoo utoke. Naye akajibu, La, sivyo; ila nitakufa papa hapa. Naye Benaya akamletea mfalme habari, akisema, Hivi ndivyo alivyonena Yoabu, na ndivyo alivyonijibu.


Mfalme akamwambia, Fanya alivyonena, umpige, ukamzike; ili uniondolee mimi na nyumba ya babangu damu aliyoimwaga Yoabu bure.


Basi mfalme akamwamuru Benaya, mwana wa Yehoyada; naye akatoka, akampiga, hata akafa. Nao ufalme ukawa imara mkononi mwa Sulemani.


Lakini, mtu akimwendea mwenziwe kwa kujikinai, kusudi apate kumwua kwa hila; huyo utamwondoa hata madhabahuni pangu, auawe.


Aliyelemewa na damu ya mtu Atalikimbilia shimo; wala mtu asimzuie.


Waueni kabisa, wazee, na viijana, na wasichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu yeyote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.


Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii Injili ya Mungu utakuwaje?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo