Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wafalme 19:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Akasema, Toka, usimame mlimani mbele za BWANA. Na tazama, BWANA akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunjavunja miamba mbele za BWANA; lakini BWANA hakuwamo katika upepo ule; na baada ya upepo, tetemeko la nchi; lakini BWANA hakuwamo katika lile tetemeko la nchi;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Nenda ukasimame mlimani, mbele yangu mimi Mwenyezi-Mungu.” Basi, Mwenyezi-Mungu akapita na kuuvumisha upepo mkali ambao uliporomosha milima na kuvunja miamba. Lakini Mwenyezi-Mungu hakuwemo katika upepo huo. Upepo ukapita, kukawa na tetemeko la ardhi. Lakini Mwenyezi-Mungu hakuwemo katika tetemeko la ardhi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Nenda ukasimame mlimani, mbele yangu mimi Mwenyezi-Mungu.” Basi, Mwenyezi-Mungu akapita na kuuvumisha upepo mkali ambao uliporomosha milima na kuvunja miamba. Lakini Mwenyezi-Mungu hakuwemo katika upepo huo. Upepo ukapita, kukawa na tetemeko la ardhi. Lakini Mwenyezi-Mungu hakuwemo katika tetemeko la ardhi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Nenda ukasimame mlimani, mbele yangu mimi Mwenyezi-Mungu.” Basi, Mwenyezi-Mungu akapita na kuuvumisha upepo mkali ambao uliporomosha milima na kuvunja miamba. Lakini Mwenyezi-Mungu hakuwemo katika upepo huo. Upepo ukapita, kukawa na tetemeko la ardhi. Lakini Mwenyezi-Mungu hakuwemo katika tetemeko la ardhi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Mwenyezi Mungu akasema, “Toka nje ukasimame juu ya mlima mbele za Mwenyezi Mungu, kwa kuwa Mwenyezi Mungu yu karibu kupita hapo.” Kisha upepo mzito na wenye nguvu ukapasua milima ile na kuvunjavunja miamba mbele za Mwenyezi Mungu, lakini Mwenyezi Mungu hakuwamo katika ule upepo. Baada ya upepo palikuwa na tetemeko la ardhi, lakini Mwenyezi Mungu hakuwamo kwenye lile tetemeko.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 bwana akasema, “Toka nje ukasimame juu ya mlima mbele za bwana, kwa kuwa bwana yu karibu kupita hapo.” Kisha upepo mwingi na wenye nguvu ukapasua milima ile na kuvunjavunja miamba mbele za bwana, lakini bwana hakuwamo katika ule upepo. Baada ya upepo palikuwa na tetemeko la nchi, lakini bwana hakuwamo kwenye lile tetemeko.

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 19:11
31 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,


Mungu wetu atakuja wala sio kimya kimya, Moto utakula mbele zake, na tufani yavuma sana ikimzunguka pande zote.


Nchi ilitetemeka Naam, mbingu zilidondoka usoni pa Mungu; Hata Sinai usoni pa Mungu; Mungu wa Israeli.


Ee Mungu, ulinyesha mvua ya neema; Urithi wako ulipochoka uliutia nguvu.


Ikawa siku ya tatu, wakati wa asubuhi, palikuwa na ngurumo na umeme, na wingu zito juu ya mlima, na sauti ya baragumu iliyolia sana. Watu wote waliokuwa kituoni wakatetemeka.


BWANA akaushukia mlima, juu ya kilele cha mlima; BWANA akamwita Musa aende hata kilele cha mlima; Musa akapanda juu.


Watu wote wakaona umeme na ngurumo na sauti ya baragumu, na ule mlima kutoka moshi; na watu walipoona hayo wakatetemeka, wakasimama mbali.


BWANA akamwambia Musa, Njoo huku juu kwangu mlimani, uwe huku; nami nitakupa vibao vya mawe na ile sheria na hiyo amri niliyoiandika ili uwafundishe.


Musa akaingia ndani ya lile wingu, akapanda mlimani; Musa akawa humo katika ule mlima siku arubaini, mchana na usiku.


Nawe uwe tayari asubuhi, ukwee juu katika mlima wa Sinai asubuhi, nawe leta nafsi yako kwangu huko katika kilele cha mlima.


BWANA akapita mbele yake, akatangaza, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;


Naye BWANA atawasikizisha watu sauti yake ya utukufu, naye atawaonesha jinsi mkono wake ushukavyo, na ghadhabu ya hasira yake, na mwako wa moto uangamizao, pamoja na dhoruba, na tufani, na mvua ya mawe ya barafu.


Nikaona, na tazama, upepo wa dhoruba ulitoka upande wa kaskazini, wingu kubwa sana, pamoja na moto, ukifanya duara ya nuru, na mwangaza pande zote, na katikati yake kitu kama rangi ya kaharabu, katikati ya moto huo.


Basi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa; hata nilipokuwa nikitoa unabii, palikuwa na mshindo mkuu; na tazama, tetemeko la nchi, na ile mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe.


BWANA si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; BWANA ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.


Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la milima yangu; kwa maana bonde lile la milima litaenea hata Aseli; naam, mtakimbia, kama vile mlivyokimbia mbele ya tetemeko la nchi, siku za Uzia, mfalme wa Yuda; na BWANA, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye.


Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la BWANA kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi.


Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali.


Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la ardhi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia.


ambaye sauti yake iliitetemesha nchi wakati ule; lakini sasa ameahidi akisema, Mara moja tena nitatetemesha si nchi tu, bali na mbingu pia.


Kisha hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la Agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua kubwa ya mawe.


Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapajawa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo.


Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.


Kukawa na tetemeko katika kambi, na katika mashamba, na katikati ya watu wote; watu wa ngomeni, na watekaji nyara, wakatetemeka nao; hata na nchi ikatetemeka pia; basi kulikuwa na tetemeko kubwa mno.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo