Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wafalme 18:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Na itakuwa, mara mimi nikiondoka kwako, Roho ya BWANA atakuchukua uende nisikojua; nami nitakapokwenda kumwambia Ahabu, naye asipokuona, ataniua, lakini mimi mtumishi wako namcha BWANA tangu ujana wangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Ninahofia kwamba mara nitakapoondoka, Roho ya Mwenyezi-Mungu itakunyakua na kukupeleka mahali nisipopajua! Nikienda kumwambia Ahabu kwamba uko hapa, naye akikutafuta asikupate, ataniua mimi, ingawaje mimi mtumishi wako nimemcha Mwenyezi-Mungu tangu ujana wangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Ninahofia kwamba mara nitakapoondoka, Roho ya Mwenyezi-Mungu itakunyakua na kukupeleka mahali nisipopajua! Nikienda kumwambia Ahabu kwamba uko hapa, naye akikutafuta asikupate, ataniua mimi, ingawaje mimi mtumishi wako nimemcha Mwenyezi-Mungu tangu ujana wangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Ninahofia kwamba mara nitakapoondoka, Roho ya Mwenyezi-Mungu itakunyakua na kukupeleka mahali nisipopajua! Nikienda kumwambia Ahabu kwamba uko hapa, naye akikutafuta asikupate, ataniua mimi, ingawaje mimi mtumishi wako nimemcha Mwenyezi-Mungu tangu ujana wangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Sijui ni wapi Roho wa Mwenyezi Mungu ataamua kukupeleka wakati nitakapokuacha. Nikienda kumwambia Ahabu na asikupate, ataniua; lakini mimi mtumishi wako nimekuwa nikimwabudu Mwenyezi Mungu tangu ujana wangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Sijui ni wapi Roho wa bwana ataamua kukupeleka wakati nitakapokuacha. Kama nikienda kumwambia Ahabu na asikupate, ataniua. Hata hivyo mimi mtumishi wako nimemwabudu bwana tangu ujana wangu.

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 18:12
27 Marejeleo ya Msalaba  

Nawe sasa wasema, Nenda, umwambie bwana wako, Tazama, Eliya yupo.


Ikawa, walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea, tazama! Kukatokea gari la moto, na farasi wa moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli.


Wakamwambia, Angalia, wako hapa pamoja nasi watumishi wako watu hamsini walio hodari; waende, twakuomba, wamtafute bwana wako; isiwe labda Roho ya BWANA imemtwaa na kumtupa juu ya mlima mmoja, au katika bonde moja. Akasema, Msiwatume.


Kwa kuwa katika mwaka wa nane wa kutawala kwake, naye akiwa bado mchanga, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi babaye; hata katika mwaka wa kumi na mbili akaanza kusafisha Yuda na Yerusalemu kwa kuondoa mahali pa juu, na kwa kuondoa Maashera, na sanamu za kuchonga, na za kusubu.


Maana ndiwe tegemeo langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu tokea ujana wangu.


Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.


Ni vizuri kwamba ulishike neno hilo; naam, hata kwa neno hilo tena usiuondoe mkono wako; kwa kuwa mtu yule amchaye Mungu atatoka katika hayo yote.


Ni nani miongoni mwenu amchaye BWANA, aitiiye sauti ya mtumishi wake? Yeye aendaye katika giza, wala hana nuru, naye alitumainia jina la BWANA, na kumtegemea Mungu wake.


Na roho hiyo ikaniinua, ikanichukua katika maono, kwa nguvu za Roho ya Mungu, hadi Ukaldayo, kwa watu wale wa uhamisho. Basi maono niliyoyaona yakaniacha.


Mkono wa BWANA ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika Roho ya BWANA, akaniweka chini, katikati ya bonde; nalo lilikuwa limejaa mifupa;


Naye akanyosha mfano wa mkono, akanishika kwa kishungi kimoja cha nywele za kichwa changu; nayo roho ikaniinua kati ya dunia na mbingu, ikanileta katika maono ya Mungu mpaka Yerusalemu, mpaka mlango wa kuingilia ua wa ndani uelekeao upande wa kaskazini; mahali palipokuwa pamewekwa sanamu ya wivu, itiayo wivu.


Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale majusi, alighadhibika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wa kiume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake kote, kuanzia wenye miaka miwili na chini yake, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale majusi.


Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.


Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.


Na Herode alipomtafuta, asimwone, aliwahoji wale walinzi, akaamuru wauawe. Kisha akateremka kutoka Yudea kwenda Kaisaria, akakaa huko.


Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi.


na ya kuwa tangu utotoni umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.


Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari, ataniua. Basi BWANA akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili kumtolea BWANA dhabihu.


Lakini Samweli alikuwa akitumika mbele za BWANA, naye alikuwa kijana aliyevaa naivera ya kitani.


Na yule mtoto, Samweli, akazidi kukua akapata kibali kwa BWANA, na kwa watu pia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo