Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wafalme 18:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Kama BWANA, Mungu wako, aishivyo, hakuna taifa wala ufalme ambao bwana wangu hakutuma watu wakutafute; na waliposema, Hayupo, akawaapisha ule ufalme, na taifa, ya kwamba hawakukuona.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Nakuapia kwa jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wako aliye hai, kwamba mfalme amekuwa akikutafuta duniani kote. Na mfalme yeyote akisema kwamba hujaonekana huko, Ahabu alimtaka huyo mfalme aape na watu wake kwamba kweli hupo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Nakuapia kwa jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wako aliye hai, kwamba mfalme amekuwa akikutafuta duniani kote. Na mfalme yeyote akisema kwamba hujaonekana huko, Ahabu alimtaka huyo mfalme aape na watu wake kwamba kweli hupo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Nakuapia kwa jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wako aliye hai, kwamba mfalme amekuwa akikutafuta duniani kote. Na mfalme yeyote akisema kwamba hujaonekana huko, Ahabu alimtaka huyo mfalme aape na watu wake kwamba kweli hupo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Hakika kama Mwenyezi Mungu, Mungu wako, aishivyo, hakuna taifa hata moja au ufalme ambapo bwana wangu hajamtuma mtu kukutafuta. Kila wakati taifa au ufalme walipodai kwamba haupo huko, aliwafanya waape kwamba hawakuweza kukupata.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Hakika kama bwana Mwenyezi Mungu wako aishivyo, hakuna taifa hata moja au ufalme ambapo bwana wangu hajamtuma mtu kukutafuta. Kila wakati taifa au ufalme walipodai kwamba haupo huko, aliwafanya waape kwamba hawakuweza kukupata.

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 18:10
20 Marejeleo ya Msalaba  

Naye mfalme akaapa, akasema, BWANA aishivyo, aliyenikomboa roho yangu katika shida zote,


Basi Eliya Mtishbi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu, Kama BWANA, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu.


Naye akasema, Kama BWANA, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie mwenyewe na mwanangu, tule kisha tufe.


Basi akaenda akafanya kama alivyosema BWANA; kwa kuwa alikwenda akakaa karibu na kijito cha Kerithi, kinachokabili Yordani.


Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe.


Nawe sasa wasema, Nenda, umwambie bwana wako, Tazama, Eliya yupo.


Eliya akasema, Kama BWANA wa majeshi aishivyo ambaye ninasimama mbele zake, hakika nitajionesha kwake leo.


Akamwambia, Nimekosa nini, hata unitie mimi mtumishi wako mkononi mwa Ahabu, aniue?


Basi kwa hiyo, BWANA aishivyo, aliyenithibitisha na kunikalisha katika kiti cha enzi cha Daudi baba yangu, akanifanyia nyumba, kama alivyoahidi, hakika atauawa leo hivi Adonia.


Mikaya akasema, Kama BWANA aishivyo, neno lile BWANA aniambialo, ndilo nitakalolinena.


Kwa kiburi chake asiye haki mnyonge anafuatiwa kwa ukali; Na wanaswe kwa hila zizo hizo walizoziwaza.


Utawasitiri kutoka kwa fitina za watu Katika maficho ya kuwapo kwako; Utawaficha katika hema Na ushindani wa ndimi.


Aketiye mahali pa siri pake Aliye Juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.


Ndipo hao wakuu wakamwambia Baruku, Nenda ukajifiche, wewe na Yeremia, wala mtu asipajue mlipo.


Mfalme akamwamuru Yerameeli, mwana wa mfalme, na Seraya, mwana wa Azrieli, na Shelemia, mwana wa Abdeeli, wamkamate Baruku, mwandishi, na Yeremia, nabii; lakini BWANA aliwaficha.


Basi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.


Chunguzeni basi, mkayajue maficho yake yote anapojificha; kisha njoni kwangu, tena msikose, nami nitakwenda pamoja nanyi; tena itakuwa, akiwapo katika nchi, mimi nitamtafutatafuta katika maelfu yote ya Yuda.


Ndipo Akishi akamwita Daudi, akamwambia, Aishivyo BWANA, wewe umekuwa mwenye adili, tena kutoka kwako na kuingia kwako pamoja nami katika jeshi ni kwema machoni pangu; kwa sababu mimi sikuona uovu ndani yako tangu siku ile uliponijia hata leo; walakini hao wakuu hawakuridhii.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo