Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wafalme 15:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 Basi Baasha wa Ahiya, wa ukoo wa Isakari, akamfanyia fitina; Baasha akampiga huko Gibethoni ulio wa Wafilisti; kwani Nadabu na Israeli wote walikuwa wakiuhusuru Gibethoni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Baasha mwana wa Ahiya, wa kabila la Isakari, akala njama dhidi ya Nadabu. Basi, wakati Nadabu na jeshi lake walipokuwa wameuzingira mji wa Gibethoni wa Wafilisti, Baasha akamvamia na kumwua,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Baasha mwana wa Ahiya, wa kabila la Isakari, akala njama dhidi ya Nadabu. Basi, wakati Nadabu na jeshi lake walipokuwa wameuzingira mji wa Gibethoni wa Wafilisti, Baasha akamvamia na kumwua,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Baasha mwana wa Ahiya, wa kabila la Isakari, akala njama dhidi ya Nadabu. Basi, wakati Nadabu na jeshi lake walipokuwa wameuzingira mji wa Gibethoni wa Wafilisti, Baasha akamvamia na kumwua,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Baasha mwana wa Ahiya wa nyumba ya Isakari akapanga njama dhidi ya Nadabu, naye akamuua huko Gibethoni, mji wa Wafilisti, wakati Nadabu na Israeli yote walikuwa wameuzingira.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Baasha mwana wa Ahiya wa nyumba ya Isakari akafanya shauri baya dhidi yake, naye akamuua huko Gibethoni, mji wa Wafilisti, wakati Nadabu na Israeli yote walipokuwa wameuzingira.

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 15:27
15 Marejeleo ya Msalaba  

Tena Bwana atajiinulia mfalme wa Israeli atakayeiharibu nyumba ya Yeroboamu siku ile; na nini tena hata sasa?


Mwaka wa tatu wa Asa mfalme wa Yuda Baasha akamwua, akatawala mahali pake.


Zimri akaingia akampiga, akamwua, katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, akatawala mahali pake.


Katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, Zimri akatawala muda wa siku saba huko Tirza. Basi, watu walikuwa wametua kambini kupigana na Gibethoni, ulio wa Wafilisti.


Na hao watu waliokuwako kambini wakasikia habari ya kwamba Zimri amekula njama, tena amemwua mfalme; kwa hiyo Israeli wote wakamfanya Omri, jemadari wa jeshi, awe mfalme juu ya Israeli siku ile kambini.


Omri akapanda kutoka Gibethoni, na Israeli wote pamoja naye, wakauhusuru Tirza.


Tena neno la BWANA likaja kwa mkono wa nabii Yehu mwana wa Hanani juu ya Baasha, na juu ya nyumba yake, kwa sababu ya mabaya yote aliyoyatenda machoni pa BWANA, akimghadhibisha kwa kazi ya mikono yake, kwa kufanana na nyumba ya Yeroboamu, na kwa sababu aliiharibu.


Na mtumwa wake Zimri, jemadari wa nusu ya magari yake, akamlia njama; alipokuwako Tirza akinywa hata kulewa nyumbani mwa Arsa, aliyekuwa juu ya nyumba huko Tirza;


Nao watumishi wake wakaondoka, wakala njama, wakamwua Yoashi katika nyumba ya Milo, hapo panaposhukia Sila.


Kwa maana Yozakari mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri, watumishi wake, wakampiga, naye akafa; wakamzika pamoja na babaze mjini mwa Daudi. Na Amazia mwanawe akatawala mahali pake.


Hivyo Yehu, mwana wa Yehoshafati, mwana wa Nimshi, akamfitinia Yoramu. Basi Yoramu alikuwa akiulinda Ramoth-Gileadi, yeye na Israeli wote, kwa sababu ya Hazaeli mfalme wa Shamu.


Hata walipoondoka kwake, (nao walimwacha ameshikwa sana na maradhi,) watumishi wake mwenyewe wakamfanyia fitina kwa ajili ya damu ya mwana wa Yehoyada kuhani, wakamwua kitandani pake, akafa; wakamzika mjini mwa Daudi, lakini hawakumzika katika makaburi ya wafalme.


Elteka, Gibethoni, Baalathi;


Tena katika kabila la Dani Elteke pamoja na mbuga zake za malisho, na Gibethoni pamoja na mbuga zake za malisho;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo