Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wafalme 11:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 Naye Hadadi aliposikia huko Misri ya kuwa Daudi amelala na babaze, na Yoabu, jemadari wa jeshi, amekufa, Hadadi akamwambia Farao, Unipe ruhusa, niende mpaka nchi yangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Lakini Hadadi aliposikia huko Misri kwamba Daudi na Yoabu mkuu wa jeshi, walikuwa wamefariki, alimwambia Farao, “Uniruhusu niondoke nirudi nchini kwangu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Lakini Hadadi aliposikia huko Misri kwamba Daudi na Yoabu mkuu wa jeshi, walikuwa wamefariki, alimwambia Farao, “Uniruhusu niondoke nirudi nchini kwangu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Lakini Hadadi aliposikia huko Misri kwamba Daudi na Yoabu mkuu wa jeshi, walikuwa wamefariki, alimwambia Farao, “Uniruhusu niondoke nirudi nchini kwangu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Alipokuwa huko Misri, Hadadi alisikia kwamba Daudi amelala na baba zake, na kwamba Yoabu aliyekuwa jemadari wa jeshi pia amekufa. Ndipo Hadadi akamwambia Farao, “Niruhusu niende ili nirudi nchi yangu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Alipokuwa huko Misri, Hadadi alisikia kwamba Daudi amepumzika na baba zake na ya kwamba pia Yoabu aliyekuwa jemadari wa jeshi amekufa. Ndipo Hadadi akamwambia Farao, “Niruhusu niende ili niweze kurudi katika nchi yangu.”

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 11:21
10 Marejeleo ya Msalaba  

Akaagana na ndugu zake, wakaenda zao; naye akawaambia, Msigombane njiani.


Kisha Abneri akamwambia Daudi, Nitaondoka, niende zangu; nami nitamkusanyia bwana wangu mfalme Israeli wote, ili wafanye agano nawe, ukamiliki juu ya wote inaowatamani roho yako. Basi Daudi akamruhusu Abneri; naye akaenda zake kwa amani.


Naye huyo dada ya Tapanesi akamzalia Genubathi mwanawe, ambaye Tapanesi alimlea nyumbani mwa Farao; naye Genubathi akawako nyumbani mwa Farao pamoja na wana wa Farao.


Farao akamwambia, Umekosa nini kwangu, hata, tazama, unatafuta kuirudia nchi yako? Akajibu, Hakuna, lakini unipe ruhusa tu.


Basi Daudi akalala na babaze, akazikwa mjini mwa Daudi.


Ndipo Benaya, mwana wa Yehoyada, akapanda, akampiga, akamwua; naye akazikwa katika nyumba yake mwenyewe iliyoko nyikani.


BWANA akamwambia Musa huko Midiani, Haya, nenda, rudi Misri; kwa kuwa wale watu wote walioutaka uhai wako wamekwisha kufa.


akasema, Inuka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto.


Naye akasema, Na iwe hivyo kama yalivyo maneno yenu. Akawatoa, nao wakaenda zao; naye akaifunga ile kamba nyekundu dirishani


Nao wakaamka alfajiri; kisha ikawa, kulipopambazuka, Samweli akamwita Sauli darini, akisema, Amka, nikusindikize urudi kwenu. Basi Sauli akainuka, nao wakatoka wote wawili, yeye na Samweli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo