Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Samueli 25:37 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

37 Ikawa asubuhi, divai ilipokuwa imemtoka Nabali, mkewe alimwambia mambo hayo, na moyo wake ukafa ndani yake, akawa kama jiwe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

37 Asubuhi, Abigaili alipoona mumewe divai imemtoka, alimweleza mambo yote, na papo hapo Nabali akapooza, akawa kama jiwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

37 Asubuhi, Abigaili alipoona mumewe divai imemtoka, alimweleza mambo yote, na papo hapo Nabali akapooza, akawa kama jiwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

37 Asubuhi, Abigaili alipoona mumewe divai imemtoka, alimweleza mambo yote, na papo hapo Nabali akapooza, akawa kama jiwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

37 Basi asubuhi, ulevi ulipokuwa umemtoka Nabali, mkewe akamwambia mambo yote, nao moyo wake ukazimia, akawa kama jiwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

37 Basi asubuhi, Nabali alipokuwa amelevuka, mkewe akamwambia mambo yote, nao moyo wake ukazimia, akawa kama jiwe.

Tazama sura Nakili




1 Samueli 25:37
7 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni;


Mungu naye awafanyie hivyo adui za Daudi, na kuzidi, nikimwachia katika wote walio wake hata mtoto mmoja wa kiume, kutakapopambazuka.


Kwa kuwa ni kweli, aishivyo BWANA, Mungu wa Israeli, aliyenizuia nisikudhuru, kwamba usingalifanya haraka kuja kunilaki, hakika huyu Nabali asingaliachiwa hata mtoto mmoja wa kiume, kutakapopambazuka.


Kisha Abigaili alimjia Nabali; na tazama, alikuwa amefanya karamu nyumbani mwake, kama karamu ya kifalme; na moyo wake huyo Nabali ukafurahiwa ndani yake, kwa maana amelewa kabisa. Kwa sababu hiyo hakumwambia neno, dogo wala kubwa, hadi kulipopambazuka.


Tena ikawa, yapata siku kumi baadaye, BWANA alimpiga huyo Nabali, hadi akafa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo