Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Samueli 10:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 na Roho ya BWANA itakujia kwa nguvu, nawe utatabiri pamoja nao, nawe utageuzwa kuwa mtu mwingine.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Roho ya Mwenyezi-Mungu itakujia kwa nguvu, nawe utaanza kutabiri pamoja nao na kugeuka kuwa mtu mwingine.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Roho ya Mwenyezi-Mungu itakujia kwa nguvu, nawe utaanza kutabiri pamoja nao na kugeuka kuwa mtu mwingine.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Roho ya Mwenyezi-Mungu itakujia kwa nguvu, nawe utaanza kutabiri pamoja nao na kugeuka kuwa mtu mwingine.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Roho wa Mwenyezi Mungu atakuja juu yako kwa nguvu, nawe utatoa unabii pamoja nao; nawe utageuzwa kuwa mtu wa tofauti.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Roho wa bwana atakuja juu yako kwa nguvu, nawe utatoa unabii pamoja nao; nawe utageuzwa kuwa mtu wa tofauti.

Tazama sura Nakili




1 Samueli 10:6
14 Marejeleo ya Msalaba  

Nami nitashuka niseme nawe huko, nami nitatwaa sehemu ya roho iliyo juu yako na kuiweka juu yao; nao watachukua mzigo wa watu hawa pamoja nawe, ili usiuchukue wewe peke yako.


Ndipo BWANA akashuka ndani ya wingu, akanena naye, akatwaa sehemu ya roho iliyokuwa juu ya Musa, akaitia juu ya wale wazee sabini; ikawa, roho hiyo ilipowashukia, wakatabiri, lakini hawakufanya hivyo tena.


Lakini watu wawili walisalia kambini, jina la mmoja aliitwa Eldadi, na jina la wa pili aliitwa Medadi; na roho ile ikawashukia; nao walikuwa miongoni mwao walioandikwa, lakini walikuwa hawakutoka kwenda hemani; nao wakatabiri kambini.


Musa akamwambia, Je! Umekuwa na wivu kwa ajili yangu; ingekuwa heri kama watu wote wa BWANA wangekuwa manabii na kama BWANA angewatia roho yake.


Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?


Roho ya BWANA ikamjia kwa nguvu, naye akampasua kana kwamba anampasua mwana-mbuzi, wala hakuwa na kitu chochote mkononi mwake; lakini hakuwaambia baba yake na mama yake aliyoyafanya.


Alipofika Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana naye; ndipo Roho ya BWANA ikamjia kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake.


Roho ya BWANA ikamjia juu yake, naye akawa mwamuzi wa Israeli; akatoka kuenda vitani, naye BWANA akamtia huyo Kushan-rishathaimu, mfalme wa Mesopotamia, mkononi mwake; na mkono wake ukamshinda Kushan-rishathaimu.


Basi, walipofika Gibea, tazama, kikosi cha manabii wakakutana naye; kisha Roho ya Mungu ikamjia kwa nguvu, naye akatabiri kati yao.


Ikawa, alipogeuka kumwacha Samweli, Mungu akambadilisha moyo; nazo ishara zile zote zikatukia siku ile ile.


Na Roho ya Mungu ikamjia Sauli kwa nguvu, hapo alipoyasikia maneno yale, na hasira yake ikawaka sana.


Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na Roho ya BWANA ikamjia Daudi kwa nguvu kuanzia siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.


Basi Sauli akatuma wajumbe ili kumkamata Daudi; nao hapo walipowaona jamaa ya manabii wakitabiri, na Samweli amesimama kama mkuu wao, Roho ya Mungu ikawajia wajumbe wa Sauli, nao pia wakatabiri.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo