Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Mambo ya Nyakati 9:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 Nao walilala kandokando nyumbani mwa Mungu, kwa kuwa ulinzi wake ulikuwa juu yao, nayo ilikuwa kazi yao kuyafungua malango kila siku asubuhi.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Wao waliishi karibu na nyumba ya Mungu kwa sababu ilikuwa ni wajibu wao kuyalinda na kuyafungua malango yake kila siku asubuhi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Wao waliishi karibu na nyumba ya Mungu kwa sababu ilikuwa ni wajibu wao kuyalinda na kuyafungua malango yake kila siku asubuhi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Wao waliishi karibu na nyumba ya Mungu kwa sababu ilikuwa ni wajibu wao kuyalinda na kuyafungua malango yake kila siku asubuhi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Walikesha mahali walipowekwa kuizunguka nyumba ya Mungu, kwa sababu iliwapasa kuilinda. Pia walitunza funguo kwa ajili ya kufungua mlango kila siku asubuhi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Walikesha mahali walipowekwa kuizunguka nyumba ya Mungu, kwa sababu iliwapasa kuilinda. Pia walitunza funguo kwa ajili ya kufungua mlango kila siku asubuhi.

Tazama sura Nakili

1 Mambo ya Nyakati 9:27
8 Marejeleo ya Msalaba  

kwa maana wale walinzi wanne, waliokuwa wakuu, nao ni Walawi, waliwajibika kuvilinda vyumba na hazina ya nyumba ya Mungu.

Na baadhi yao walivilinda vyombo vya huduma; kwani huingizwa kwa hesabu, na kutolewa kwa hesabu vile vile.

Njoni, enyi watumishi wote wa BWANA, Mhimidini BWANA Ninyi mnaohudumu usiku Katika nyumba ya BWANA.

nikawaleta ndani ya nyumba ya BWANA, ndani ya chumba cha wana wa Hanani, mwana wa Igdalia, mtu wa Mungu, kilichokuwa karibu na chumba cha wakuu, nacho kilikuwa juu ya chumba cha Maaseya, mwana wa Shalumu, bawabu;

Laiti angekuwapo kwenu mtu mmoja wa kuifunga milango; msije mkawasha moto bure madhabahuni pangu! Sina furaha kwenu, asema BWANA wa majeshi, wala sitakubali dhabihu yoyote mikononi mwenu.

ikiwa ni huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;

Naye Samweli akalala hadi asubuhi, akaifungua milango ya nyumba ya BWANA. Samweli akaogopa kumjulisha Eli maono hayo.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo