Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 9:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

22 Hao wote waliochaguliwa kuwa walinzi wa malango walikuwa watu mia mbili na kumi na wawili. Nao wakahesabiwa kwa nasaba katika vijiji vyao, ambao Daudi na Samweli, huyo mwonaji, walikuwa wamewaweka katika kazi yao waliyotegemewa kwayo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Jumla, watu 212 walichaguliwa kuwa walinzi wa maingilio ya hekalu. Waliandikishwa kulingana na vijiji walimoishi. Mfalme Daudi na Samueli mwonaji ndio waliowathibitisha katika wadhifa huu muhimu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Jumla, watu 212 walichaguliwa kuwa walinzi wa maingilio ya hekalu. Waliandikishwa kulingana na vijiji walimoishi. Mfalme Daudi na Samueli mwonaji ndio waliowathibitisha katika wadhifa huu muhimu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Jumla, watu 212 walichaguliwa kuwa walinzi wa maingilio ya hekalu. Waliandikishwa kulingana na vijiji walimoishi. Mfalme Daudi na Samueli mwonaji ndio waliowathibitisha katika wadhifa huu muhimu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Jumla ya waliochaguliwa kuwa mabawabu katika sakafu za kupuria nafaka walikuwa watu mia mbili na kumi na wawili (212). Waliandikishwa kwa koo zao kwenye vijiji vyao. Mabawabu hawa waliwekwa katika nafasi zao za kuaminiwa na Daudi, pamoja na Samweli aliyekuwa mwonaji.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Jumla ya waliochaguliwa kuwa mabawabu katika sakafu za kupuria nafaka walikuwa watu 212. Waliandikishwa kwa koo zao kwenye vijiji vyao. Mabawabu hawa waliwekwa katika nafasi zao za kuaminiwa na Daudi pamoja na mwonaji Samweli.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 9:22
18 Marejeleo ya Msalaba  

tena kuhusu zamu za makuhani na Walawi, na ya kazi yote ya huo utumishi wa nyumba ya BWANA, na ya vyombo vyote vya utumishi nyumbani mwa BWANA;


Na tazama, hizo zamu za makuhani na Walawi ziko, kwa utumishi wote wa nyumba ya Mungu; nao watakuwapo pamoja nawe kwa kazi ya kila namna, kila mtu mwenye hiari, aliye stadi kwa utumishi wowote; tena maofisa na watu wote watakuwa chini ya amri yako kabisa.


Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo hadi mwisho, angalia, zimeandikwa katika kumbukumbu za Samweli, mwonaji, na katika kumbukumbu za Nathani, nabii, na katika kumbukumbu za Gadi, mwonaji;


na Obadia, mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni; na Berekia, mwana wa Asa, mwana wa Elkana; waliokaa katika vijiji vya Wanetofathi.


Basi watu hao na wana wao walikuwa na kazi ya ulinzi wa malango ya nyumba ya BWANA, yaani, nyumba ya maskani, kwa zamu.


Naye Matithia, Mlawi mmojawapo, aliyekuwa mzaliwa wa kwanza wa Shalumu, Mkora, aliwajibika kusimamia uokaji wa mikate myembamba.


Akawaweka walinzi malangoni pa nyumba ya BWANA, asiingie aliye najisi kwa namna yoyote.


Na chini yake walikuwa Edeni, na Minyamini, na Yeshua, na Shemaya, na Amaria, na Shekania, mijini mwa makuhani, kwa walivyoaminiwa, ili kuwagawia ndugu zao kwa zamu, wakuu na wadogo sawasawa;


na wale waliohesabiwa kwa nasaba ya wadogo wao wote, wake zao, na wana wao, na binti zao, katika kusanyiko lote; kwani kwa vile walivyoaminiwa, wakajitakasa katika utakatifu;


Na wa Walawi, wengine walikaa katika Yuda na wengine katika Benyamini.


Na siku hiyo watu wakaagizwa juu ya vyumba vya hazina, kwa sadaka za kuinuliwa, na kwa malimbuko, na kwa zaka, ili kuzikusanya, kwa kadiri ya mashamba ya miji, sehemu zilizoamriwa katika torati za makuhani, na Walawi; kwa maana Yuda waliwafurahia makuhani na Walawi waliotumika.


(Hapo zamani katika Israeli, mtu alipokwenda kuuliza neno kwa Mungu, husema hivi, Haya! Twende kwa mwonaji; maana mtu aitwaye sasa Nabii hapo zamani aliitwa Mwonaji.)


Tufuate:

Matangazo


Matangazo