Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 6:71 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

71 Na wana wa Gershoni wakapewa, katika jamaa ya nusu kabila ya Manase; Golani katika Bashani pamoja na viunga vyake, na Ashtarothi pamoja na viunga vyake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

71 Jamaa za ukoo wa Gershomu walipewa miji ifuatayo pamoja na malisho yake: Katika nusu ya kabila la Manase walipewa: Golani katika Bashani pamoja na malisho yake, Ashtarothi pamoja na malisho yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

71 Jamaa za ukoo wa Gershomu walipewa miji ifuatayo pamoja na malisho yake: Katika nusu ya kabila la Manase walipewa: Golani katika Bashani pamoja na malisho yake, Ashtarothi pamoja na malisho yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

71 Jamaa za ukoo wa Gershomu walipewa miji ifuatayo pamoja na malisho yake: katika nusu ya kabila la Manase walipewa: Golani katika Bashani pamoja na malisho yake, Ashtarothi pamoja na malisho yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

71 Wagershoni walipokea miji ifuatayo: Katika nusu ya kabila la Manase, walipokea Golani katika Bashani, na pia Ashtarothi, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

71 Wagershoni walipokea miji ifuatayo pamoja na maeneo yake ya malisho: Katika nusu ya kabila la Manase: walipewa Golani katika Bashani na pia Ashtarothi.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 6:71
9 Marejeleo ya Msalaba  

na katika nusu kabila ya Manase; Taanaki pamoja na viunga vyake, na Ibleamu pamoja na viunga vyake; kwa mabaki ya jamaa ya wana wa Kohathi.


na katika kabila la Isakari; Kishioni pamoja na viunga vyake, na Daberathi pamoja na viunga vyake;


alipokwisha kumpiga Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akikaa Heshboni, na Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa akikaa Ashtarothi iliyo katika Edrei;


nayo ni hii, Beseri ya barani iliyo katika nchi tambarare, kwa Wareubeni; na Ramothi iliyo Gileadi, kwa Wagadi; na Golani iliyo Bashani, kwa Wamanase.


na nusu ya Gileadi, na Ashtarothi, na Edrei, hiyo miji ya ufalme wa Ogu katika Bashani, ilikuwa ni ya wana wa Makiri mwana wa Manase maana, kwa hiyo nusu ya wana wa Makiri sawasawa na jamaa zao.


Tena ng'ambo ya pili ya Yordani pande za Yeriko upande wa kuelekea mashariki wakaweka Bezeri ulioko nyikani, katika nchi tambarare ya kabila la Reubeni, na Ramothi katika Gileadi katika kabila la Gadi, na Golani katika Bashani katika kabila la Manase.


Tena wana wa Gershoni, katika jamaa za Walawi, waliwapa, katika hiyo nusu ya kabila la Manase, Golani katika Bashani pamoja na mbuga zake za malisho, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji; na Beeshtera pamoja na mbuga zake za malisho; miji miwili.


Tena wana wa Gershoni walipata kwa kura miji kumi na mitatu katika jamaa za kabila la Isakari, na katika kabila la Asheri, na katika kabila la Naftali, na katika hiyo nusu ya kabila la Manase huko Bashani.


na habari ya hayo yote aliyowatenda wale wafalme wawili wa Waamori, waliokuwa huko ng'ambo ya pili ya Yordani, maana huyo Sihoni, mfalme wa Heshboni, na Ogu, mfalme wa Bashani, aliyekuwa huko Ashtarothi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo