Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 6:62 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

62 Na wana wa Gershoni walipewa kwa kura miji kumi na mitatu, kulingana na jamaa zao, katika kabila la Isakari, na katika kabila la Asheri, na katika kabila la Naftali, na katika kabila la Manase waliokaa Bashani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

62 Ukoo wa Gershomu, kulingana na jamaa zake ulipewa miji kumi na mitatu katika kabila la Isakari, na katika kabila la Naftali na katika kabila la Manase katika Bashani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

62 Ukoo wa Gershomu, kulingana na jamaa zake ulipewa miji kumi na mitatu katika kabila la Isakari, na katika kabila la Naftali na katika kabila la Manase katika Bashani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

62 Ukoo wa Gershomu, kulingana na jamaa zake ulipewa miji kumi na mitatu katika kabila la Isakari, na katika kabila la Naftali na katika kabila la Manase katika Bashani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

62 Wazao wa Gershoni, kufuatana na koo zao, walipewa miji kumi na tatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali, na kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

62 Wazao wa Gershoni, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na mitatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 6:62
9 Marejeleo ya Msalaba  

Na ndugu zao, Walawi, ndio waliowekwa ili kufanya huduma yote ya maskani ya nyumba ya Mungu.


Nao waliobaki wa wana wa Kohathi walipewa kwa kura miji kumi, katika jamaa ya kabila hilo, yaani, nusu kabila, nusu ya Manase.


Na wana wa Merari walipewa kwa kura miji kumi na miwili, kulingana na jamaa zao, katika kabila la Reubeni, na katika kabila la Gadi, na katika kabila la Zabuloni.


Huyo akamzalia mtoto wa kiume, akamwita jina lake Gershomu, maana alisema, Nimekuwa mgeni katika nchi ya ugeni.


na mpaka ukafikia hadi Tabori, na Shahasuma na Beth-shemeshi; na mwisho wa mpaka wao ulikuwa katika mto wa Yordani; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.


Tena wana wa Gershoni walipata kwa kura miji kumi na mitatu katika jamaa za kabila la Isakari, na katika kabila la Asheri, na katika kabila la Naftali, na katika hiyo nusu ya kabila la Manase huko Bashani.


Na wana wa Merari kwa kufuata jamaa zao walipata miji kumi na miwili katika kabila la Reubeni, na katika kabila la Gadi, na katika kabila la Zabuloni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo