Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 6:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

32 Nao wakafanya kazi yao ya kuimba mbele ya maskani ya hema ya kukutania, hata Sulemani alipokuwa amejenga ile nyumba ya BWANA huko Yerusalemu; nao wakatoa huduma yao kwa kufuata zamu zao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Walifanya kazi yao ya kuimba mbele ya hema takatifu la mkutano hadi wakati mfalme Solomoni alipojenga hekalu la Mwenyezi-Mungu huko Yerusalemu. Waliutekeleza wajibu wao barabara, kwa zamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Walifanya kazi yao ya kuimba mbele ya hema takatifu la mkutano hadi wakati mfalme Solomoni alipojenga hekalu la Mwenyezi-Mungu huko Yerusalemu. Waliutekeleza wajibu wao barabara, kwa zamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Walifanya kazi yao ya kuimba mbele ya hema takatifu la mkutano hadi wakati mfalme Solomoni alipojenga hekalu la Mwenyezi-Mungu huko Yerusalemu. Waliutekeleza wajibu wao barabara, kwa zamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, hadi hapo Mfalme Sulemani alipojenga Hekalu la Mwenyezi Mungu huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Sulemani alipojenga Hekalu la bwana huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 6:32
20 Marejeleo ya Msalaba  

na Yohana akamzaa Azaria (ndiye huyo aliyefanya kazi ya ukuhani katika nyumba aliyoijenga Sulemani huko Yerusalemu)


Na hawa ndio watu aliowaweka Daudi kwenye kazi ya kuimba katika nyumba ya BWANA, sanduku lile lilipopata mahali pa kukaa.


Na hawa ndio waliohudumu pamoja na wana wao. Katika wana wa Wakohathi; Hemani mwimbaji, mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli;


Tena hawa ndio waimbaji, wakuu wa koo za baba zao katika Walawi, ambao walikaa vyumbani, kisha walikuwa hawana kazi nyingine; kwa kuwa walifanya kazi yao mchana na usiku.


Hezekia akaziweka zamu za makuhani na Walawi kwa zamu zao, kila mtu kwa kadiri ya huduma yake, makuhani na Walawi pia, kwa sadaka za kuteketezwa na kwa sadaka za amani, kutumika, na kushukuru, na kusifu, malangoni mwa kambi ya BWANA.


Nao waimbaji, wana wa Asafu wakasimama mahali pao, kama alivyoamuru Daudi, na Asafu, na Hemani, na Yeduthuni mwonaji wa mfalme; nao mabawabu walikuwa katika kila lango; hawakuhitaji kuondoka katika huduma yao, kwa kuwa ndugu zao Walawi wakawaandalia.


Wakawaweka makuhani katika sehemu zao, wakawaweka na Walawi katika zamu zao, kwa ajili ya huduma ya Mungu, iliyokuwako Yerusalemu; kama ilivyoandikwa katika chuo cha Musa.


Tena nje ya lango la ndani palikuwa na vyumba kwa waimbaji, katika ua wa ndani, uliokuwa kando ya lango lililoelekea kaskazini, navyo vilikabili upande wa kusini; na kimoja kando ya lango lililoelekea upande wa mashariki, kilikabili upande wa kaskazini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo