Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 6:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

31 Na hawa ndio watu aliowaweka Daudi kwenye kazi ya kuimba katika nyumba ya BWANA, sanduku lile lilipopata mahali pa kukaa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 Hawa ndio watu ambao mfalme Daudi aliwaweka wahudumu kama waimbaji katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, baada ya sanduku la agano kuwekwa ndani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 Hawa ndio watu ambao mfalme Daudi aliwaweka wahudumu kama waimbaji katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, baada ya sanduku la agano kuwekwa ndani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 Hawa ndio watu ambao mfalme Daudi aliwaweka wahudumu kama waimbaji katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, baada ya sanduku la agano kuwekwa ndani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 Hawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 Hawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya bwana, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 6:31
16 Marejeleo ya Msalaba  

Wakaliingiza sanduku la BWANA, na kuliweka mahali pake, katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake, naye Daudi akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za BWANA.


Wakalipandisha sanduku la BWANA, na ile hema ya kukutania, na vyombo vitakatifu vyote vilivyokuwa katika ile Hema; vitu hivyo makuhani na Walawi wakavipandisha.


Basi Daudi akajijengea nyumba katika mji wa Daudi; akatayarisha mahali kwa ajili ya sanduku la Mungu, akalipigia hema.


Basi Daudi, na wazee wa Israeli, na makamanda wa maelfu, wakaenda, ili kulipandisha sanduku la Agano la BWANA kutoka nyumbani mwa Obed-edomu kwa furaha kuu;


Naye Daudi alikuwa amevaa joho la kitani safi, na Walawi wote waliolichukua sanduku, na waimbaji, na Kenania msimamizi wa uchukuzi, na waimbaji; naye Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.


na mwanawe huyo ni Shimea, na mwanawe huyo ni Hagla, na mwanawe huyo ni Asaya.


Nao wakafanya kazi yao ya kuimba mbele ya maskani ya hema ya kukutania, hata Sulemani alipokuwa amejenga ile nyumba ya BWANA huko Yerusalemu; nao wakatoa huduma yao kwa kufuata zamu zao.


Tena hawa ndio waimbaji, wakuu wa koo za baba zao katika Walawi, ambao walikaa vyumbani, kisha walikuwa hawana kazi nyingine; kwa kuwa walifanya kazi yao mchana na usiku.


Hata wajenzi walipouweka msingi wa hekalu la BWANA, wakawaweka makuhani, wamevaa mavazi yao, wenye baragumu, na Walawi, wana wa Asafu, wenye matoazi, ili wamhimidi BWANA, kama alivyoagiza Daudi, mfalme wa Israeli.


Hapo ndipo mahali pangu pa raha milele, Hapo nitakaa kwa maana nimepatamani.


Ee BWANA, uinuke, uende kwenye raha yako, Wewe na sanduku la nguvu zako.


Tena nje ya lango la ndani palikuwa na vyumba kwa waimbaji, katika ua wa ndani, uliokuwa kando ya lango lililoelekea kaskazini, navyo vilikabili upande wa kusini; na kimoja kando ya lango lililoelekea upande wa mashariki, kilikabili upande wa kaskazini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo