Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 6:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

3 Na wana wa Amramu; Haruni, na Musa, na Miriamu. Na wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Amramu alikuwa na wana wawili: Aroni na Mose, na binti mmoja jina lake Miriamu. Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Amramu alikuwa na wana wawili: Aroni na Mose, na binti mmoja jina lake Miriamu. Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Amramu alikuwa na wana wawili: Aroni na Mose, na binti mmoja jina lake Miriamu. Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Amramu alikuwa na wana: Haruni, Musa, na Miriamu. Haruni alikuwa na wana: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Amramu alikuwa na wana: Haruni, Musa, na Miriamu. Haruni alikuwa na wana: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 6:3
18 Marejeleo ya Msalaba  

wa wana wa Uzieli; Aminadabu mkuu wao, na nduguze mia moja kumi na wawili.


Wana wa Kohathi; Amramu, Ishari, Hebroni, na Uzieli, watu wanne.


Wana wa Amramu; Haruni na Musa; naye Haruni akatengwa, ili ayatakase yaliyo matakatifu sana, yeye na wanawe milele, ili kufukiza uvumba mbele za BWANA, kumtumikia, na kubariki kwa jina lake, milele.


Wa Waishari, Shelomothi; wa wana wa Shelomothi, Yahathi.


Na wana wa Kohathi; Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli.


Eleazari akamzaa Finehasi; na Finehasi akamzaa Abishua;


Na Miriamu, nabii mwanamke, dada yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza.


Dada yake mtoto akasimama mbali ili ajue yatakayompata.


Basi dada yake mtoto akamwambia binti Farao, Je! Niende nikamwite mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kwako, akunyonyeshee mtoto huyu?


Kisha BWANA akamwambia Musa, Kweeni wewe, na Haruni, na Nadabu, na Abihu, na watu sabini wa wazee wa Israeli, mkamfikie BWANA; mkasujudie kwa mbali;


Nawe umlete Haruni ndugu yako karibu nami, na wanawe pamoja naye, miongoni mwa wana wa Israeli, ili anitumikie katika kazi ya ukuhani. Haruni, na Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari, wana wa Haruni.


Huyo Amramu akamwoa Yokebedi shangazi yake; naye akamzalia Haruni, na Musa; na miaka ya maisha yake Amramu ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na saba.


Haruni akamwoa Elisheba, binti ya Aminadabu, dada yake Nashoni; naye akamzalia Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.


Na Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, wakatwaa kila mtu chetezo chake, wakatia moto ndani yake, wakatia na uvumba, nao wakatoa moto najisi mbele ya BWANA, ambao yeye hakuwaagiza.


Kisha Musa akanena na Haruni, na Eleazari, na Ithamari, hao wanawe waliobaki, Twaeni hiyo sadaka ya unga iliyosalia katika kafara za BWANA zilizotolewa kwa moto, mkaile pasipo kutiwa chachu, pale karibu na madhabahu; kwa kuwa ni takatifu sana;


Kisha Musa akamtafuta sana huyo mbuzi wa sadaka ya dhambi, naye, tazama, alikuwa amekwisha kuteketezwa; naye akawakasirikia hao Eleazari na Ithamari, wana wa Haruni, hao waliobaki, akawaambia,


Kwa maana nilikupandisha kutoka nchi ya Misri, na kukukomboa utoke katika nyumba ya utumwa, nami niliwatuma Musa, na Haruni, na Miriamu, watangulie mbele yako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo