Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 6:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 na Yehosadaki akachukuliwa mateka, hapo BWANA alipowachukua mateka Yuda na Yerusalemu, kwa mkono wa Nebukadneza.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Yehosadaki alikwenda uhamishoni wakati Mwenyezi-Mungu alipowapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa kuutumia mkono wa mfalme Nebukadneza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Yehosadaki alikwenda uhamishoni wakati Mwenyezi-Mungu alipowapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa kuutumia mkono wa mfalme Nebukadneza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Yehosadaki alikwenda uhamishoni wakati Mwenyezi-Mungu alipowapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa kuutumia mkono wa mfalme Nebukadneza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Yehosadaki alihamishwa wakati Mwenyezi Mungu aliwapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Mfalme Nebukadneza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Yehosadaki alihamishwa wakati bwana aliwapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Mfalme Nebukadneza.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 6:15
17 Marejeleo ya Msalaba  

Wala BWANA hakusema ya kwamba atalifuta jina la Israeli litoke chini ya mbingu; lakini akawaokoa kwa mkono wa Yeroboamu mwana wa Yehoashi.


Na kamanda wa askari walinzi akamtwaa Seraya, kuhani mkuu, na Sefania, kuhani wa pili, na wale walinzi watu wa mlango;


Naye mfalme wa Babeli akawapiga, na kuwaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Hivyo Yuda wakachukuliwa utumwani kutoka nchi yao.


na Azaria akamzaa Seraya; na Seraya akamzaa Yehosadaki;


Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari.


Ndipo akaondoka Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yosadaki, wakaanza kuijenga nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu; na pamoja nao walikuwa manabii wa Mungu, wakiwasaidia.


Akasema, Ee Bwana, nakuomba, tuma kwa mkono wake huyo utakayemtuma.


Basi, Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, akawachukua mateka mabaki ya watu waliosalia katika mji mpaka Babeli, na hao pia waliouacha mji na kujiunga naye, na mabaki ya watu waliosalia.


Watu hawa ndio wale ambao Nebukadneza aliwachukua mateka; katika mwaka wa saba, Wayahudi elfu tatu na ishirini na watatu;


Katika mwaka wa pili wa utawala wa mfalme Dario, mwezi wa sita, siku ya kwanza ya mwezi, neno la BWANA lilimjia Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, kwa kinywa chake nabii Hagai, kusema,


Ndipo Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, pamoja na hao watu wote waliokuwa wamebaki, wakaitii sauti ya BWANA, Mungu wao, na maneno ya nabii Hagai, kama BWANA, Mungu wao, alivyomtuma; nao watu wakaogopa mbele za BWANA.


BWANA akaiamsha roho ya Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na roho ya Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na roho za watu waliokuwa wamebaki; wakaenda, wakafanya kazi katika nyumba ya BWANA wa majeshi, Mungu wao;


Sema sasa na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na hao watu waliokuwa wamebaki, ukisema,


Hata walipofika wakalikutanisha kanisa, wakawaeleza mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwamba amewafungulia Mataifa mlango wa imani.


Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yangu, Mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo