Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 5:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

26 Naye Mungu wa Israeli akamwamsha roho Pulu, mfalme wa Ashuru, yaani roho ya Tiglath-Pileseri, mfalme wa Ashuru, naye akawachukua mateka hao Wareubeni, na Wagadi, na nusu kabila ya Wamanase; akawaleta mpaka Hala, na Habori, na Hara, na mpaka mto wa Gozani, hata siku hii ya leo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Basi, Mungu wa Israeli akamfanya Pulu, mfalme wa Ashuru, (ambaye pia alijulikana kama Tiglath-pileseri), aivamie nchi yao na kuwachukua mateka hao Wareubeni, Wagadi na nusu Manase ya mashariki mpaka uhamishoni huko Hala, Habori na Hara, kando ya mto Gozani, ambako wamekaa mpaka leo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Basi, Mungu wa Israeli akamfanya Pulu, mfalme wa Ashuru, (ambaye pia alijulikana kama Tiglath-pileseri), aivamie nchi yao na kuwachukua mateka hao Wareubeni, Wagadi na nusu Manase ya mashariki mpaka uhamishoni huko Hala, Habori na Hara, kando ya mto Gozani, ambako wamekaa mpaka leo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Basi, Mungu wa Israeli akamfanya Pulu, mfalme wa Ashuru, (ambaye pia alijulikana kama Tiglath-pileseri), aivamie nchi yao na kuwachukua mateka hao Wareubeni, Wagadi na nusu Manase ya mashariki mpaka uhamishoni huko Hala, Habori na Hara, kando ya mto Gozani, ambako wamekaa mpaka leo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Kwa hiyo Mungu wa Israeli akaiamsha roho ya Pulu, mfalme wa Ashuru (ambaye pia alijulikana kama Tiglath-Pileseri), ambaye aliwachukua Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase kwenda uhamishoni. Akawapeleka huko Hala, Habori, Hara na mto Gozani, ambako wamekaa hadi leo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Kwa hiyo Mungu wa Israeli akaiamsha roho ya Pulu, mfalme wa Ashuru (ambaye pia alijulikana kama Tiglath-Pileseri), ambaye aliwachukua Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase kwenda uhamishoni. Akawapeleka huko Hala, Habori, Hara na mto Gozani, ambako wamekaa mpaka leo.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 5:26
18 Marejeleo ya Msalaba  

Tena hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, akamchochea Daudi juu yao, akisema, Nenda, ukawahesabu watu wa Israeli na Yuda.


Akaja Pulu mfalme wa Ashuru juu ya nchi; naye Menahemu akampa Pulu talanta elfu moja za fedha, ili kwamba mkono wake uwe pamoja naye, na ufalme uwe imara mkononi mwake.


Katika siku za Peka mfalme wa Israeli akaja Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akatwaa Iyoni, na Abel-beth-maaka, na Yanoa, na Kedeshi, na Hazori, na Gileadi, na Galilaya, nchi yote ya Naftali; akawahamisha hao watu mpaka Ashuru.


Basi Ahazi akatuma wajumbe kwa Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akasema, Mimi ni mtumishi, tena mwana wako; kwea, ukaniokoe mkononi mwa mfalme wa Shamu, na mkononi mwa mfalme wa Israeli, walioniinukia.


Katika mwaka wa tisa wa Hoshea, huyo mfalme wa Ashuru akautwaa Samaria, akawahamisha Israeli mpaka Ashuru, akawaweka katika Hala na Habori, karibu na mto wa Gozani, na katika miji ya Wamedi.


Mfalme wa Ashuru akawahamisha Israeli mpaka Ashuru, akawaweka katika Hala, na katika Habori, karibu na mto wa Gozani, na katika miji ya Wamedi;


Je! Miungu ya mataifa wale, ambao baba zangu waliwaangamiza, imewaokoa? Yaani, Gozani, na Harani, na Resefu, na wana wa Adini waliokuwa katika Telasari?


Kwani walianguka wengi waliouawa, kwa sababu vita vile vilikuwa vya Mungu. Nao wakakaa katika nchi yao hadi wakati wa ule uhamisho.


na mwanawe huyo ni Beera, ambaye Tiglath-Pileseri, mfalme wa Ashuru, alimchukua mateka; ndiye aliyekuwa mkuu wa Wareubeni.


Hivyo Israeli wote walihesabiwa kwa nasaba; na tazama, hizo zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli; na Yuda wakachukuliwa mateka mpaka Babeli, kwa sababu ya makosa yao.


Na Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru akamjia, akamfadhaisha, asimtie nguvu kwa lolote.


Matarishi, kwa amri ya mfalme na maofisa wake wakapeleka nyaraka katika Israeli na Yuda yote, kusema, Enyi wana wa Israeli, mrudieni BWANA, Mungu wa Abrahamu, na Isaka, na Israeli, apate kuwarudia ninyi mlionusurika na kuokoka toka mikononi mwa Wafalme wa Ashuru.


Kwa hiyo BWANA akaleta juu yao makamanda wa jeshi la mfalme wa Ashuru, waliomkamata Manase kwa minyororo, wakamfunga kwa pingu, wakamchukua mpaka Babeli.


Ndipo wakaondoka wakuu wa koo za mababa, wa Yuda na Benyamini, na makuhani, na Walawi, naam, watu wote ambao Mungu ameamsha roho zao kukwea, ili kuijenga nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu.


Je! Miungu ya mataifa, ambao baba zangu waliwaangamiza, wamewaokoa? Gozani, na Harani, na Resefu, na wana wa Adini waliokuwa katika Telasari?


Ni kweli, BWANA, wafalme wa Ashuru wameziharibu nchi zote, na mashamba yao,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo