Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Mambo ya Nyakati 28:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Ndipo Daudi akampa Sulemani mwanawe mfano wa ukumbi wa hekalu, na nyumba zake, na hazina zake, na ghorofa zake, na vyumba vyake vya ndani, na mahali pa kiti cha rehema;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Ndipo Daudi akampa Solomoni mwanawe ramani ya majengo yote ya hekalu, nyumba zake, hazina zake, ghorofa zake, vyumba vyake vya ndani na mahali pa kiti cha rehema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Ndipo Daudi akampa Solomoni mwanawe ramani ya majengo yote ya hekalu, nyumba zake, hazina zake, ghorofa zake, vyumba vyake vya ndani na mahali pa kiti cha rehema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Ndipo Daudi akampa Solomoni mwanawe ramani ya majengo yote ya hekalu, nyumba zake, hazina zake, ghorofa zake, vyumba vyake vya ndani na mahali pa kiti cha rehema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Ndipo Daudi akampa Sulemani mwanawe kielelezo kwa ajili ya ukumbi wa Hekalu, nyumba zake, vyumba vyake vya hazina, ghorofa zake, vyumba vyake vya ndani na mahali pa kufanyia upatanisho.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Ndipo Daudi akampa Sulemani mwanawe kielelezo kwa ajili ya ukumbi wa Hekalu, nyumba zake, vyumba vyake vya hazina, ghorofa zake, vyumba vyake vya ndani na mahali pa kufanyia upatanisho.

Tazama sura Nakili

1 Mambo ya Nyakati 28:11
28 Marejeleo ya Msalaba  

Akavijenga vyumba mbavuni mwa nyumba yote, kwenda juu kwake kila kimoja kilikuwa mikono mitano; vikaitegemea nyumba kwa boriti za mwerezi.

Na ukumbi mbele ya hekalu la nyumba, urefu wake ulikuwa mikono ishirini, kadiri ya upana wa nyumba; na upana wake mikono kumi mbele ya nyumba.

na mfano wa yote aliyokuwa nao rohoni, kuhusu nyua za nyumba ya BWANA, na ya vyumba vyote vilivyoizunguka, ya hazina za nyumba ya Mungu, na ya hazina za vitu vilivyowekwa wakfu;

Hayo yote, akasema Daudi, yamenielea kwa maandiko kutoka kwa mkono wa BWANA, naam, kazi zote za mfano huu.

Makuhani wakaliingiza sanduku la Agano la BWANA mahali pake katika chumba cha ndani cha nyumba, patakatifu pa patakatifu, yaani, chini ya mabawa ya makerubi.

alikuwa amemtengenezea chumba kikubwa, hapo walipoweka zamani sadaka za unga, na ubani, na vyombo, na zaka za nafaka, na divai, na mafuta, walivyoamriwa kuwapa Walawi, na waimbaji, na mabawabu; tena sadaka za kuinuliwa zilizokuwa za makuhani.

Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama mfano wake, uliooneshwa mlimani.

Sawasawa na haya yote nikuoneshayo, mfano wa maskani, na mfano wa samani zake zote, ndivyo mtakavyovifanya.

Nawe utaisimamisha hiyo maskani sawasawa na mfano wake uliooneshwa mlimani.

Nenda nyumbani kwa Warekabi, ukanene nao, ukawalete nyumbani kwa BWANA, katika chumba kimoja, ukawape divai wanywe.

Na toka mahali palipo mbele ya lango, penye maingilio yake, hata mahali palipo mbele ya ukumbi wa ndani ya lango, dhiraa hamsini.

Akainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina.

watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule uliooneshwa katika mlima.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo