Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 27:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

23 Lakini Daudi hakufanya hesabu ya waliokuwa na umri wa chini ya miaka ishirini; kwa kuwa BWANA alikuwa amesema, ya kwamba atawaongeza Israeli mfano wa nyota za mbinguni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Mfalme Daudi hakuwahesabu wale waliokuwa chini ya umri wa miaka ishirini kwa maana Mwenyezi-Mungu aliahidi kuwaongeza Waisraeli wawe wengi kama nyota za mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Mfalme Daudi hakuwahesabu wale waliokuwa chini ya umri wa miaka ishirini kwa maana Mwenyezi-Mungu aliahidi kuwaongeza Waisraeli wawe wengi kama nyota za mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Mfalme Daudi hakuwahesabu wale waliokuwa chini ya umri wa miaka ishirini kwa maana Mwenyezi-Mungu aliahidi kuwaongeza Waisraeli wawe wengi kama nyota za mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Daudi hakuwahesabu watu waliokuwa chini ya miaka ishirini, kwa sababu Mwenyezi Mungu alikuwa ameahidi kuwafanya Israeli kuwa wengi kama nyota za angani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Daudi hakuwahesabu watu waliokuwa chini ya miaka ishirini, kwa sababu bwana alikuwa ameahidi kuwafanya Israeli kuwa wengi kama nyota za angani.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 27:23
7 Marejeleo ya Msalaba  

Akamtoa nje, akasema, Tazama juu mbinguni kisha uzihesabu nyota, kama unaweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.


katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki lango la adui zao;


Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia.


Tena hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, akamchochea Daudi juu yao, akisema, Nenda, ukawahesabu watu wa Israeli na Yuda.


nao waliwakutanisha watu wote, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, nao wakaonesha ukoo wa vizazi vyao kwa kufuata jamaa zao, kwa nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, mmoja mmoja.


Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, naye alikuwa kama mfu, watu wengi kama nyota za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufuoni, usioweza kuhesabika.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo