1 Mambo ya Nyakati 27:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC1 Basi wana wa Israeli kwa hesabu yao, wakuu wa koo za mababa, na makamanda wa maelfu na wa mamia, na wasimamizi wao waliomtumikia mfalme, kwa neno lolote la zamu za kuingia na za kutoka mwezi kwa mwezi, miezi yote ya mwaka, wa kila zamu, walikuwa watu elfu ishirini na nne. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema1 Hii ndiyo orodha ya wakuu wa wazawa wa Israeli waliokuwa viongozi wa jamaa, na makamanda wa maelfu na mamia na maofisa wao waliomtumikia mfalme Daudi kuhusu zamu za kuingia na kutoka. Kila mwezi kila mwaka, kundi tofauti la watu 24,000 walilishika zamu ya kufanya kazi. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND1 Hii ndiyo orodha ya wakuu wa wazawa wa Israeli waliokuwa viongozi wa jamaa, na makamanda wa maelfu na mamia na maofisa wao waliomtumikia mfalme Daudi kuhusu zamu za kuingia na kutoka. Kila mwezi kila mwaka, kundi tofauti la watu 24,000 walilishika zamu ya kufanya kazi. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza1 Hii ndiyo orodha ya wakuu wa wazawa wa Israeli waliokuwa viongozi wa jamaa, na makamanda wa maelfu na mamia na maofisa wao waliomtumikia mfalme Daudi kuhusu zamu za kuingia na kutoka. Kila mwezi kila mwaka, kundi tofauti la watu 24,000 walilishika zamu ya kufanya kazi. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu1 Hii ndiyo orodha ya Waisraeli: viongozi wa jamaa, majemadari wa maelfu, majemadari wa mamia na maafisa wao, waliomtumikia mfalme kwa lolote lililohusu vikosi vya jeshi vilivyokuwa zamu mwezi baada ya mwezi katika mwaka mzima. Kila kikosi kimoja kilikuwa na watu elfu ishirini na nne. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu1 Hii ndiyo orodha ya Waisraeli: viongozi wa jamaa, majemadari wa maelfu, majemadari wa mamia na maafisa wao, waliomtumikia mfalme kwa lolote lililohusu vikosi vya jeshi vilivyokuwa zamu mwezi baada ya mwezi katika mwaka mzima. Kila kikosi kimoja kilikuwa na watu 24,000. Tazama sura |
Kisha Daudi akawakusanya huko Yerusalemu wakuu wote wa Israeli, wakuu wa kabila, na makamanda wa vikosi wenye kumtumikia mfalme kwa zamu, na makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, na wenye kutawala juu ya mali na milki za mfalme, na za wanawe, pamoja na matowashi, na mashujaa, naam, wanaume mashujaa wote.