Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 24:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 Ndivyo walivyogawanyika kwa kura, wao kwa wao; kwani kulikuwa na wakuu wa patakatifu, na watumishi wa Mungu, wa wana wa Eleazari, na wa wana wa Ithamari pia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Waligawanywa kwa kura kwani kulikuwa na wakuu wa mahali patakatifu na viongozi wa kidini miongoni mwa koo zote mbili, yaani ukoo wa Eleazari na ukoo wa Ithamari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Waligawanywa kwa kura kwani kulikuwa na wakuu wa mahali patakatifu na viongozi wa kidini miongoni mwa koo zote mbili, yaani ukoo wa Eleazari na ukoo wa Ithamari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Waligawanywa kwa kura kwani kulikuwa na wakuu wa mahali patakatifu na viongozi wa kidini miongoni mwa koo zote mbili, yaani ukoo wa Eleazari na ukoo wa Ithamari.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Waliwagawanya bila upendeleo kwa kupiga kura, kwa kuwa kulikuwa na maafisa wa mahali patakatifu na maafisa wa Mungu miongoni mwa wazao wale wa Eleazari na wale wa Ithamari.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Waliwagawanya bila upendeleo kwa kupiga kura, kwa kuwa kulikuwa na maafisa wa mahali patakatifu na maafisa wa Mungu miongoni mwa wazao wale wa Eleazari na wale wa Ithamari.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 24:5
17 Marejeleo ya Msalaba  

Hao nao wakapigiwa kura vile vile, kama ndugu zao wana wa Haruni, machoni pa Daudi mfalme, na Sadoki, na Ahimeleki, na wakuu wa koo za baba za makuhani na za Walawi; koo za baba za mkuu, vile vile kama za nduguye mdogo.


Wakaonekana wakuu wengi wa wana wa Eleazari kuliko wa wana wa Ithamari; wakagawanyika hivi; wa wana wa Eleazari kulikuwa na kumi na sita, waliokuwa wakuu wa koo za baba zao; na wa wana wa Ithamari, kulingana na koo za baba zao, wanane.


Wakapigiwa kura ya huduma zao, kwa pamoja, mdogo kwa mkubwa, mwalimu kwa mwanafunzi.


Nao wakapigiwa kura kwa ajili ya kila lango, wadogo na wakubwa kwa pamoja, kwa kufuata koo za baba zao.


na Azaria, mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu, mkuu wa nyumba ya Mungu;


Na wakuu wake wakawapa watu, na makuhani na Walawi matoleo ya hiari. Hilkia na wana na Yehieli, wakubwa wa nyumba ya Mungu, wakawapa makuhani, kuwa matoleo ya Pasaka, wana-kondoo elfu mbili na mia sita, na ng'ombe mia tatu.


na Seraya, mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu, msimamizi wa nyumba ya Mungu,


Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini hukumu zake zote ni za BWANA.


Kwa hiyo nitawatia unajisi wakuu wa patakatifu, nami nitamfanya Yakobo kuwalaani, na Israeli kuwa tukano.


Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, na tupige kura, tupate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga kura, nayo kura ikamwangukia Yona.


Wakati ule wakuu wa makuhani, na wazee wa watu, wakakusanyika katika behewa ya Kuhani Mkuu, jina lake Kayafa;


Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumwua;


Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja.


Hata walipokuwa wakisema na watu wale, makuhani na walinzi wa hekalu na Masadukayo wakawatokea,


na Anasi Kuhani Mkuu, na Kayafa pia, na Yohana na Iskanda, na wote wale waliokuwa jamaa zake Kuhani Mkuu.


Basi mlinzi mkuu wa hekalu na wakuu wa makuhani waliposikia haya, wakaingiwa na shaka kwa ajili yao, litakuwaje jambo hilo.


Kisha Yoshua akapiga kura kwa ajili yao hapo mbele za BWANA katika Shilo; huko Yoshua akawagawanyia wana wa Israeli hiyo nchi sawasawa na mafungu yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo