Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Mambo ya Nyakati 24:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Wakaonekana wakuu wengi wa wana wa Eleazari kuliko wa wana wa Ithamari; wakagawanyika hivi; wa wana wa Eleazari kulikuwa na kumi na sita, waliokuwa wakuu wa koo za baba zao; na wa wana wa Ithamari, kulingana na koo za baba zao, wanane.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Kwa vile ambavyo kulipatikana viongozi wanaume wengi zaidi miongoni mwa wazawa wa Ithamari, waliwagawanya wazawa wa Eleazari chini ya viongozi kumi na sita, na wazawa wa Ithamari chini ya viongozi wanane.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Kwa vile ambavyo kulipatikana viongozi wanaume wengi zaidi miongoni mwa wazawa wa Ithamari, waliwagawanya wazawa wa Eleazari chini ya viongozi kumi na sita, na wazawa wa Ithamari chini ya viongozi wanane.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Kwa vile ambavyo kulipatikana viongozi wanaume wengi zaidi miongoni mwa wazawa wa Ithamari, waliwagawanya wazawa wa Eleazari chini ya viongozi kumi na sita, na wazawa wa Ithamari chini ya viongozi wanane.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Idadi kubwa ya viongozi walipatikana miongoni mwa wazao wa Eleazari, kuliko miongoni mwa wazao wa Ithamari, nao waligawanywa kwa uwiano: Viongozi kumi na sita kutoka jamaa ya wazao wa Eleazari na viongozi wanane kutoka jamaa ya wazao wa Ithamari.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Mambo ya Nyakati 24:4
7 Marejeleo ya Msalaba  

Hao walikuwa wana wa Lawi, kwa kufuata koo za baba zao, yaani, vichwa vya koo za baba zao waliohesabiwa, kwa hiyo hesabu ya majina yao, hao walioifanya kazi ya utumishi wa nyumba ya BWANA, wenye miaka ishirini na zaidi.

Akawagawanya Daudi, na Sadoki wa wana wa Eleazari, na Ahimeleki wa wana wa Ithamari, katika utumishi kwa kadiri ya huduma yao.

Ndivyo walivyogawanyika kwa kura, wao kwa wao; kwani kulikuwa na wakuu wa patakatifu, na watumishi wa Mungu, wa wana wa Eleazari, na wa wana wa Ithamari pia.

Sulemani akawaita Israeli wote, na makamanda wa maelfu, na wa mamia, na waamuzi, na kila kiongozi wa Israeli, na wakuu wa familia.

Na siku za Yoyakimu wakawako makuhani, wakuu wa mbari za mababa; wa Seraya, Meraya; wa Yeremia, Hanania;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo