Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 24:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Na zamu za wana wa Haruni ni hizi. Wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Hayo ndiyo makundi ya wazawa wa Aroni. Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Hayo ndiyo makundi ya wazawa wa Aroni. Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Hayo ndiyo makundi ya wazawa wa Aroni. Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Hii ndiyo migawanyo ya wazao wa Haruni: Haruni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Hii ndiyo migawanyo ya wana wa Haruni: Haruni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 24:1
16 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Daudi akawagawanya kwa zamu zao sawasawa na wana wa Lawi; Gershoni, Kohathi, na Merari.


tena kuhusu zamu za makuhani na Walawi, na ya kazi yote ya huo utumishi wa nyumba ya BWANA, na ya vyombo vyote vya utumishi nyumbani mwa BWANA;


Na wana wa Amramu; Haruni, na Musa, na Miriamu. Na wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.


mwana wa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu;


Basi Walawi na Yuda wote wakafanya kama alivyowaamuru Yehoyada kuhani; wakawatwaa kila mtu watu wake, hao watakaoingia siku ya sabato, na wale watakaotoka siku ya sabato; kwa maana Yehoyada kuhani hakuwaruhusu waondoke.


Hezekia akaziweka zamu za makuhani na Walawi kwa zamu zao, kila mtu kwa kadiri ya huduma yake, makuhani na Walawi pia, kwa sadaka za kuteketezwa na kwa sadaka za amani, kutumika, na kushukuru, na kusifu, malangoni mwa kambi ya BWANA.


Ikawa makuhani walipokwisha kutoka katika patakatifu; (kwani makuhani wote waliokuwapo, walikuwa wamejitakasa, wala hawakuzishika zamu zao;


Akaziamuru, kulingana na agizo la Daudi babaye, zamu za makuhani za kutumika, nao Walawi kwa kadiri ya malinzi yao, ili kusifu, na kuhudumu mbele ya makuhani, kama ilivyohitajiwa kila siku; tena mabawabu kwa zamu zao za kila mlango; maana ndivyo alivyoamuru Daudi mtu wa Mungu.


Wakawaweka makuhani katika sehemu zao, wakawaweka na Walawi katika zamu zao, kwa ajili ya huduma ya Mungu, iliyokuwako Yerusalemu; kama ilivyoandikwa katika chuo cha Musa.


mwana wa Abishua, mwana wa Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni, kuhani mkuu;


Nawe umlete Haruni ndugu yako karibu nami, na wanawe pamoja naye, miongoni mwa wana wa Israeli, ili anitumikie katika kazi ya ukuhani. Haruni, na Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari, wana wa Haruni.


Haruni akamwoa Elisheba, binti ya Aminadabu, dada yake Nashoni; naye akamzalia Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.


Tena kwake Haruni walizaliwa hawa, Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.


Tena majina ya hao wana wa Haruni ni haya; Nadabu mzaliwa wa kwanza, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.


Kisha Nadabu na Abihu walikufa mbele za BWANA, waliposongeza moto wa kigeni mbele za BWANA, katika jangwa la Sinai, nao walikuwa hawana wana; na Eleazari na Ithamari wakafanya kazi ya ukuhani wakati wa uhai wa Haruni baba yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo