Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 23:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 Basi Daudi akawagawanya kwa zamu zao sawasawa na wana wa Lawi; Gershoni, Kohathi, na Merari.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Daudi aliwagawanya Walawi katika makundi matatu kulingana na koo za kabila la Lawi: Ukoo wa Gershoni, ukoo wa Kohathi na ukoo wa Merari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Daudi aliwagawanya Walawi katika makundi matatu kulingana na koo za kabila la Lawi: Ukoo wa Gershoni, ukoo wa Kohathi na ukoo wa Merari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Daudi aliwagawanya Walawi katika makundi matatu kulingana na koo za kabila la Lawi: ukoo wa Gershoni, ukoo wa Kohathi na ukoo wa Merari.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Daudi akawagawa Walawi katika makundi kufuatana na wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Daudi akawagawa Walawi katika makundi kufuatana na wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 23:6
18 Marejeleo ya Msalaba  

Wa Wagershoni; Ladani, na Shimei.


Na zamu za wana wa Haruni ni hizi. Wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.


Kwa zamu zao mabawabu; wa Wakora; Meshelemia mwana wa Kore, wa wana wa Ebiasafu.


tena kuhusu zamu za makuhani na Walawi, na ya kazi yote ya huo utumishi wa nyumba ya BWANA, na ya vyombo vyote vya utumishi nyumbani mwa BWANA;


Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari.


Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari.


Yehoyada akauamuru usimamizi wa nyumba ya BWANA chini ya mkono wa makuhani Walawi, aliowagawa Daudi nyumbani mwa BWANA, ili wazisongeze sadaka za kuteketezwa za BWANA, kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, kwa kufurahi na kuimba, kama alivyoamuru Daudi.


Akawasimamisha Walawi nyumbani mwa BWANA wenye matoazi, wenye vinanda, na wenye vinubi, kama alivyoamuru Daudi, na Gadi mwonaji wa mfalme, na Nathani nabii; kwani BWANA aliamuru hivi kwa manabii wake.


Hezekia akaziweka zamu za makuhani na Walawi kwa zamu zao, kila mtu kwa kadiri ya huduma yake, makuhani na Walawi pia, kwa sadaka za kuteketezwa na kwa sadaka za amani, kutumika, na kushukuru, na kusifu, malangoni mwa kambi ya BWANA.


Hivyo huduma ikatengenezwa, wakasimama makuhani mahali pao, na Walawi kwa zamu zao, kama alivyoamuru mfalme.


Mkajiweke tayari kwa kadiri ya nyumba za baba zenu, kwa zamu zenu, kama alivyoandika Daudi mfalme wa Israeli, na kama alivyoandika Sulemani mwanawe.


Akaziamuru, kulingana na agizo la Daudi babaye, zamu za makuhani za kutumika, nao Walawi kwa kadiri ya malinzi yao, ili kusifu, na kuhudumu mbele ya makuhani, kama ilivyohitajiwa kila siku; tena mabawabu kwa zamu zao za kila mlango; maana ndivyo alivyoamuru Daudi mtu wa Mungu.


Wakawaweka makuhani katika sehemu zao, wakawaweka na Walawi katika zamu zao, kwa ajili ya huduma ya Mungu, iliyokuwako Yerusalemu; kama ilivyoandikwa katika chuo cha Musa.


Na wana wa Lawi walikuwa ni hawa kwa majina yao; Gershoni, na Kohathi, na Merari.


Hayo ndiyo majina ya wana wa Haruni, hao makuhani waliotiwa mafuta, ambao aliwaweka wakfu ili wafanye kazi ya ukuhani.


Huu ndio utumishi wa wana wa Kohathi katika hema ya kukutania, katika vile vyombo vitakatifu sana;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo