Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 23:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 Maana kwa maneno ya mwisho ya Daudi, hao wana wa Lawi walihesabiwa, wenye miaka ishirini na zaidi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Kulingana na maagizo ya mwisho aliyotoa Daudi, Walawi wote waliofikia umri wa miaka ishirini waliandikishwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Kulingana na maagizo ya mwisho aliyotoa Daudi, Walawi wote waliofikia umri wa miaka ishirini waliandikishwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Kulingana na maagizo ya mwisho aliyotoa Daudi, Walawi wote waliofikia umri wa miaka ishirini waliandikishwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Kulingana na maagizo ya mwisho ya Daudi, Walawi walihesabiwa kuanzia umri wa miaka ishirini au zaidi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Kulingana na maagizo ya mwisho ya Daudi, Walawi waliohesabiwa ni wale wa kuanzia umri wa miaka ishirini au zaidi.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 23:27
9 Marejeleo ya Msalaba  

Basi haya ndiyo maneno ya mwisho ya Daudi. Daudi, mwana wa Yese, anena, Anena huyo mtu aliyeinuliwa juu, Yeye, masihi wake Mungu wa Yakobo, Mtungaji wa nyimbo za Israeli mwenye kupendeza;


Hao walikuwa wana wa Lawi, kwa kufuata koo za baba zao, yaani, vichwa vya koo za baba zao waliohesabiwa, kwa hiyo hesabu ya majina yao, hao walioifanya kazi ya utumishi wa nyumba ya BWANA, wenye miaka ishirini na zaidi.


wala Walawi hawahitaji tena kuichukua maskani, na vyombo vyake vyote kwa utumishi wake.


Kwani kazi yao ilikuwa kuwangojea wana wa Haruni katika utumishi wa nyumba ya BWANA, nyuani, na vyumbani, na kwa kuvisafisha vitakatifu vyote, ndiyo kazi ya utumishi wa nyumba ya Mungu;


Nao wakahesabiwa Walawi wenye miaka thelathini na zaidi; na jumla yao kwa vichwa, mtu kwa mtu, ikawa elfu thelathini na nane.


na wale waliohesabiwa kwa nasaba ya makuhani kufuata nyumba za baba zao, na Walawi, wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, katika sehemu yao, kwa kadiri ya zamu zao;


Maombi ya Daudi mwana wa Yese, yamekwisha.


Nao watavitunza vyombo vyote vya hema ya kukutania, na kuwatumikia wana wa Israeli, kwa kuhudumu katika maskani.


tangu waliopata umri wa miaka thelathini na zaidi hata umri wa miaka hamsini, wote waingiao katika utumishi huo, ili kufanya kazi ya hema ya kukutania.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo