Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 23:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

25 Kwa kuwa Daudi alisema, BWANA, Mungu wa Israeli, amewastarehesha watu wake; naye hukaa Yerusalemu milele;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Daudi alisema, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, amewapa watu wake amani, naye ataishi Yerusalemu milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Daudi alisema, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, amewapa watu wake amani, naye ataishi Yerusalemu milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Daudi alisema, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, amewapa watu wake amani, naye ataishi Yerusalemu milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Kwa maana Daudi alikuwa amesema, “Kwa vile Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, amewapa watu wake amani, na amekuja kuishi Yerusalemu milele,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Kwa maana Daudi alikuwa amesema, “Kwa vile bwana, Mungu wa Israeli amewapa watu wake raha na amekuja kuishi Yerusalemu milele,

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 23:25
18 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa, mfalme alipokuwa akikaa katika nyumba yake, hapo BWANA alipomstarehesha, asiudhiwe na adui zake waliomzunguka pande zote,


naam, kama ilivyokuwa tangu siku ile nilipowaamuru waamuzi, wawe juu ya watu wangu Israeli; nami nitakustarehesha mbele ya adui zako wote. Tena BWANA anakuambia ya kwamba BWANA atakujengea nyumba.


Hakika nimekujengea nyumba ya kukaa, iwe mahali pa makao yako milele.


Lakini Mungu je? Hakika atakaa juu ya nchi? Tazama, mbingu hazikutoshi, wala mbingu za mbingu; sembuse nyumba hii niliyoijenga!


Je! Si BWANA, Mungu wenu, aliye pamoja nanyi? Na kuwapa amani pande zote? Kwa kuwa wenyeji wa nchi amewatia mkononi mwangu; nayo nchi imetiishwa mbele za BWANA, na mbele ya watu wake.


Yehoyada akauamuru usimamizi wa nyumba ya BWANA chini ya mkono wa makuhani Walawi, aliowagawa Daudi nyumbani mwa BWANA, ili wazisongeze sadaka za kuteketezwa za BWANA, kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, kwa kufurahi na kuimba, kama alivyoamuru Daudi.


Na ahimidiwe BWANA toka Sayuni, Akaaye Yerusalemu. Haleluya.


Enyi milima mirefu, kwani kuutazama kwa wivu Mlima alioutamani Mungu akae juu yake? Naam, BWANA atakaa juu yake milele.


Wewe umepaa juu, umeteka mateka, Umepewa vipawa katikati ya wanadamu; Naam, hata na wakaidi, BWANA Mungu akae nao.


Mwimbieni BWANA akaaye Sayuni, Yatangazeni kwa watu matendo yake.


Angalieni, mimi na watoto hawa niliopewa na BWANA tu ishara na ajabu katika Israeli, zitokazo kwa BWANA wa majeshi, yeye akaaye katika mlima Sayuni.


Kuuzunguka ni mianzi elfu kumi na nane; na jina la mji huo tangu siku hiyo litakuwa hili, BWANA yupo.


Nami nitaitakasa damu yao ambayo sijaitakasa; kwa maana BWANA ndiye akaaye Sayuni.


BWANA asema hivi, Mimi nimerudi Sayuni, nami nitakaa katikati ya Yerusalemu; na Yerusalemu utaitwa, Mji mwaminifu; na mlima wa BWANA wa majeshi utaitwa, mlima mtakatifu.


Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.


Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.


Hata ikawa baada ya siku nyingi, BWANA alipokuwa amekwisha kuwapa Israeli amani mbele ya adui zao pande zote, naye Yoshua alipokuwa mzee, mwenye miaka mingi sana,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo